Kibao kikionesha Kijiji cha Chiwanda Wilaya ya Momba anakoishi mwanamke aliyejifungua mapacha wanne. |
Msafara wa kuelekea Nyumbani kwa Mama wanne ukiwa unacha Lami barabara ya Sumbawanga Tunduma. |
Baada ya kuwasili nyumbani kwa Mama Wanne, Moja ya wakurugenzi wa Mbeya yetu Joseph Mwaisango ambaye alikuwa ni kiongozi wa Msafara akionesha baadhi ya zawadi zilizopelekwa. |
Baadhi ya watoto na wakazi wa kijiji cha Chiwanda wakisaidia kushusha mizigo kwenye gari huku wakionesha kufurahia misaada hiyo. |
Erick Mwaisango akimkabidhi moja ya zawadi Mama Wanne kwa niaba ya Kampuni ya Nora SilverBoutique ya Jijini Dar Es Salaam. |
Familia ya mama wanne ikiwa katika picha ya Pamoja na baadhi ya Wenyeviti wa Kijiji na kitongoji baada ya kupokea Msaada kutoka kwa Wasamaria wema waliowakilishwa na Joseph na Erick Mwaisango. |
Baba Wanne Webson Simkanga na mkewe Aida Nakawala wakiwa wamewabeba watoto wao. |
Wanahabari Venance Matinya wa gazeti la Jamboleo na Ezekiel Kamanga wa Bomba fm Redio wakichukua maoni kutoka kwa Baba Wanne. |
Mapacha wanne kutoka kulia ni Asifiwe, Daudi,Anania na Alinikumbu wakionesha nyuso za furaha ikiwa ni ishara ya kuimarika kwa afya zao. |
Baba na Mama wanne wakifurahia misaada iliyotolewa na wasamaria wema kwa ajili ya familia yao.
WATOTO wanne waliozaliwa
na mama mmoja kwa mkupuo (Quadruplets) usiku wa kuamkia Mwaka mpya wa 2014
katika Hospitali ya Wazazi ya META jijini Mbeya wanaendelea vizuri.
Watoto hao walizaliwa na Aida Nakawala (25) mkazi wa kijiji
cha Chiwanda, Wilaya ya Momba, Mkoa wa Mbeya, ambaye amewashukuru wasamaria
wema kwa kuendelea kuwapa misaada iliyosaidia watoto hao kukua vizuri.
Akizungumza na www.mbeyayetu.blogspot.com
Nyumbani kwao jana Baba Mzazi wa
watoto hao, Webson Simkanga(28) alisema yeye binafsi hana uwezo kiuchumi lakini
kutokana misaada mbali mbali aipatayo kutoka kwa wasamaria wema inasaidia
kuimarisha afya za watoto wake.
Alisema hivi sasa Watoto wake hao wamekua
vizuri na kuleta matumaini kutokana na hali zao za kiafya na kuchangamka sana kinyume
na matarajio ya watu wengi wasiokuwa na mapenzi mema kwa familia hiyo wakiombea
mabaya kuwatokea.
Alisema kutokana na kuimarika kwa afya
zao baba huyo ametoa majina kwa watoto wake hao huku akitarajia kuwabatiza kama
ishara ya Wakristu ya kuwakabidhi watoto hao mikononi mwa Kanisa na Mungu.
Aliwataja majina watoto hao kuanzia wa
kwanza hadi wa Mwisho kuwa ni Alinikumbu(mtoto mwenye huruma), Daudi, Asifiwe na Anania ambao anatarajia
kuwabatiza Machi 9, Mwaka huu katika kanisa la African Mission Church(AMC).
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji cha
Chiwanda, Ignas Sinkara, alisema jukumu la kijiji bado lipo palepale
kuhakikisha hali za watoto zinaendelea kuimarika siku hadi siku na kuongeza
kuwa pia Wasamaria wema wanazidi kujitokeza kuwachangia familia hiyo.
Alisema mbali na wanakijiji kujitokeza
kwa wingi kumsaidia mama wanne kubeba watoto na kusaidia kazi za nyumbani
taasisi zingine bado zinatoa misaada yao likiwemo Kanisa Katoliki ambalo
lilichangia Fedha tyaslimu Shilingi 56,000/= pamoja na Debe mbili za Mahindi na
kusaidia kuandaa shamba la kupanda Mihogo la Familia hiyo.
Aidha katika Ziara ya Waandishi wa habari
Kijijini hapo yenye lengo la kutaka kuwajulia hali watoto hao ikiwa ni pmoja na
kuwasilisha michango mbali mbali
iliyotolewa na wasamaria wema kwa ajili ya familia hiyo.
Misaada hiyo ni pamoja na Msaada
uliopokelewa ba Mtandao wa kijamii wenye makao yake makuu Jijini Dar Es Salaam
wa www.michuzi.blogspot.com ulipokea kutoka
kwa Msamaria mwema wa Uingereza, Bi Gladness Sariah, ambaye alitoa maboksi
mawili yenye nguo na vitu kadhaa vya watoto.
Msamaria mwema mwingine aliyejulikana kwa Norah
SilverBoutique toka DSM ambaye ametoa Maziwa Lactogen Dazan Mbili yaani
makopo 24 pamoja na nguo vyenye thamani ya zaidi ya Shilingi Laki Tano.
Pia Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA)
Kanda ya Nyanda za Juu Kusini iliwezesha usafiri kwa wanahabari hao kwa kuchangia
Mafuta, Serengeti Freight Forwarders ya huko Uingereza na ofisi za Michuzi
Media Group (MMG) kuwezesha kufika
kwa mizigo hiyo Jijini Mbeya.
Na Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment