Baadhi ya waadishi wa habari
Akizungumza na waandishi wa habari
katika ukumbi wa Hospitali ya Rufaa ya Mbeya, katibu wa Hospitali hiyo, Aisha
Mtanda alisema kuwa bonanza hilo ambalo litabeba ujumbe usemao,HUDUMA BORA INAWEZEKANA KWA PAMOJA TUMETHUBUTU TUMEWEZA NA TUNASONGA MBELE. limeandaliwa na Uongozi wa hospitali hiyo kwa kushirikiana
na kampuni ya Bia TBL na kwamba bonanza hili
litafanyika siku ya Jumamosi(February 8, mawaka huu).
Alisema kuwa lengo la bonanza hilo
ni kufanya hafla fupi kwa watumsihi wa Hospitali hiyo kwa kuaga mwaka wa 2013 na kuukalibisha mwaka mpya wa 2014, ambalo pia litafanyikia katika viwanja vya
Chuo cha Uhasibu (TIA)tawi la Mbeya.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa sherehe Christopher Mwakibombaki alisema katika Bonanza hilo
kutakuwa na michezo mbali mbali kama vile mpia wa miguu, mpira wa pete,
Netboli, Basketi boli, Voleboli, kuvuta kamba, kukimbia kwenye magunia,kukuna
nazi na mashindano ya kula.
Aliongeza kuwa taasisi
zinazotarajia kushiriki ni pamoja na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,
Halmashauri ya Jiji, kampuni ya Saruji Mbeya, Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya, Madiwani wa Halmashauri wa
Jiji, Kampuni ya Bia (TBL), Hospitali ya Rufaa na kitengo cha Benki ya damu
salama.
Na Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment