MKUU wa Mkoa wa Mbeya,Abbas Kandoro, ameviagiza, Chama cha
Mapinduzi (CCM)mkoa na chama cha
soka(Mrefa) kukutana na kuweka njia bora ya kukusanya michango ya fedha
inayotolewa na wadau kwa ajili ya kazi ya upandaji nyasi katika wa Sokoine,
baada ya kuibuka hisia za ubadhirifu wa fedha hizo.
Alitoa Agizo hilo baada ya kutembelea uwanjani hapo, hatua
hiyo imekuja ikiwa ni siku chache baada ya Clouds fm kutangaza habari iliyomtaka kuingilia kati zoezi
hilo la upandaji nyasi baada ya kuonekana kusuasua.
Kandoro baada ya kufika uwanjani hapo na kukuta kazi ikisuasua,
aliomba maelezo ya kina kutoka kwa viongozi wa CCM na Mrefa, pamoja na sababu
zinazokwamisha kazik hiyo kufanyika kwa ufanisi ili kuendana na ratiba ya bodi
ya ligi iliyoamuru kufungiwa kwa uwanja huo kutokana na kasoro nyingi.
Akitoa maelezo, M wenyekiti wa CCM mkoa, Godfrey Zambi, alisema zoiezi hilo limeendelea
kusuasua kutokana na kukosekana nguvu kazi ya kutosha na usimamizi duni wa
shughulli hiyo.
“Mkuu wa mkoa kule ndani ya kikao tulipata maelezo ambayo yako
tofauti na hali tuliyoikuta hapas na kwa hali hii kuna uwezekano ikasababisha
watu kukosa kuona mechi katika mzunguko wa pili” alilalamika kwa hasira Zambi.
Kabla ya Zambi kumaliza kutoa maelezo, ghafla mafundi
waliokuwepo uwanjani hapo walikatiza maezo na kuanza kulalamika kutolipwa fedha
zao, pamoja na sababu nyingine zinazokwamisha kuendelea kufanyika kwa haraka
kwa zoezi hilo.
“Mfano leo tumekosa kabisa nyasi za kupanda….maana wanakijiji
wamezuia mzigo wa nyasi zilizokatwa usib ebwe mpaka walipwe fedha zao , jambo
ambalo limekwamisha zoezi zima” alisema mmoja wa vibarua haol.
Kibarua mwingine alisema walilazimika kuhama kijiji cha wali
walikokuwa wakichimba nyasi hizo na kuhamia kungine kutokana na serikali ya
kijiji kuchachamaa kutokana na kutolipwa fedha zao za wiki mbili zilizopita.
Kutokana na maelezo hayo ya vibarua, Mkuu wa Mkoa aliwatataka
Mkurugenzi wa Jiji, Mussa
Nzungiza, na viongozi wa chama cha soka watoe majibu.
Hata hivyo katika hali iliyojaa mkanganyiko, Mkurugenzi wa Jiji
alisema kuwa wao wamekuwa wakitoa fedha kila siku kadiri ya Mrefa wanavyopeleka
mahitaji, jambo lililopingwa hapo hapo na M akamu mwenyekiti wa Mrefa,Omary
Mahinya.
“Mkuu wa Mkoa naomba niweke sawa maelezo ya mkurugenzi, sisi
kama Mrefa hatujapekea fedha hizo, kwani sisi tulichofanywa ni kmuk,opeshwa
kiasi cha shilingi milioni tano na TFF(Shirikisho la soka hapa nchiniP)”
alifafanua Mahinya na kumshangaza mkuu wa mkoa.
Baada ya kuona sarakasi zinaendelea katika maelezo hayo, ndipo
Mkuu wa Mkoa aliamua kutoa agizo “kuanzia sasa naomba CCM na mrefa make chini
na kupan ga utaratibu mzuri wa hizi fedha na mimi naahidi kufuatilia hatua kwa
hatua, haiwezekani mtuharibie mambo hapa” alihitimisha Kandoro.
Hata hivyo katika kuonesha kuguswa na hali hiyo, MKandoro
alianzisha ziara ya kushitukmiza hadi katika vijiji zinakochimbwa nyasi hizo
umbali wa kilometa 40, ambapo Alikutana na malalamiko ya wananchi kutolipwa
fedha zao kiasi cha shilingi 600,000 na kuamua kutoa nusu ya fedha hizo na
kuwaahidi kiasi kilichobaki kulipwa ndani ya siku mbili.
Siku chache zilizopita, Mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa
Mbeya, elius Mwanjala, alisema zoezi hilo lingekamilika leo baada ya kupata
kiasi cha shilingi milioni 8 kati ya 10 walizokuwa wakizihitaji.
Hata hivyo, Mkuu wa Mkoa Kandoro alipokea ombi la wadau la
kutaka kazi ya upandaji nyasi ichukuliwe na Jeshi la kujenga Taifa (JKT) kwa
kushirikiana na wataalamu kmwa kuahidi kulifanyia kazi haraka iwezekanavyo.
Kwa upande wake, mtaalam wa kupanda nyasi ndani ya uwanja huo,
Siddy Ibrahim , alisema kama yale yalioashidiwa na viongozi yatatekelezwa na
hadi kufikia Januari 3 zoezi likakamilika, uwezekano wa wa mechi za mzunguko wa
pili kuchezewa katika uwanja huo utakuwepo.
Na Moses Ng’wat,Mbeya.
Picha na Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment