KAMPUNI ya Citysign
Promotion & Markerting Agency Limited ya Jijini Mbeya inatarajia kuandaa
ligi ya mpira wa miguu itayohusisha timu za madereva wa pikipiki maarufu
bodaboda za Jiji la Mbeya.
Hayo yamebainishwa na
mmoja wa wakurugenzi wa kampuni hiyo, Geophrey Mwangunguru katika kikao cha
maandalizi baina yao na viongozi wa chama cha waendesha bodaboda kilichofanyika
katika viwanja vya City pub Jijini Mbeya.
Mwaangungulu alisema
lengo la kuandaa ligi hiyo ni kuwaunganisha madereva wa bodaboda ili kusudi waweze
kutambuliwa na wanajamii ambao asilimia kubwa wamekuwa wakiwatuhumu
kwamba ni wakorofi waliokosa ustarabu na umoja.
Alisema kupitia ligi
hiyo wataweza kupata faida kubwa kwa kupatiwa elimu mbalimbali zikiwemo usalama
barabarani ili kupunguza ajali zisizokuwa za lazima,kuunganishwa na mifuko ya
jamii, bima za afya,saccos na jinsi ya kujiwekea akiba.
Aliongeza kuwa ligi
hiyo intarajiwa kuanza kulindima mapema mwezi wa nne baada taratibu zote
kukamilika kwa kuzihusisha timu zaidi ya 30 ambazo ni timu tano kutoka kanda
sita za vituo vya bodaboda.
Kwa upande wake
Mwenyekiti wa kamati ya ufundi wa shirikisho la mpira wa miguu Jiji la
Mbeya(MUFA) Ramadhani Lulandala alisema ni vema madereva wa bodaboda
wakajiandaa vizuri huku wakitambua sheria na kanuni za mpira wa miguu kwa
kuepuka kuwafanyia vurugu waamuzi na kwamba atakayebainika atachukuliwa hatua
kali za kisheria.
Aidha kwa upande wao
viongozi wa boda boda wakiongozwa na Mwenyekiti wao Vicent Mwashoma na katibu
Msumba Mdesa waliwapongeza waandaaji wa ligi hiyo kwa kuwakumbuka waendesha
bodaboda na kuwahakikishia kushiriki ligi hiyo kwa amani na kwamba haina haja
ya kulihusisha jeshi la polisi kwa madai kuwa wanauwezo wa kudhibitina wao
wenyewe.
Na Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment