Mchungaji
Edward Mtweve wa kanisa la Tanzania Assemblies of God[TAG]Uyole Njia Panda
amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya Waendesha pikipiki[Bodaboda]kuvuruga
ibada ya mazishi ya mwendesha pikipiki aitwaye Gabriel Osward Ngalele.
Vurugu hizo
zilitokea katika Kanisa hilo baada ya Gabriel Ngalele kufariki kwa ajali ya
gari Januari 13 majira ya saa 11 alfajiri eneo la SAE akiwa na abiria wake
ambapo walifariki papo hapo baada ya kugongwa na Roli.
Taratibu za
mazishi zilipokamilika mwili wa marehemu ulipelekwa katika Kanisa hilo wakati
mchungaji akiendesha Ibada aliomba utulivu kwa wafiwa ambapo walitulia lakini
vijana zaidi ya 300 waendesha bodaboda walilipuka kwa kelele hali ilyomfanya
mchungaji kuomba utulivu katika Ibada.
Hata hivyo
vijana hao waliendelea kujaa katika kanisa hilo na kukosekana utulivu hali
iliyomlazimu mchungaji kuwaambia kama wamekosa utulivu basi watakuwa wamefuata
ubwabwa katika msiba huo hali iliyofanya kutokea mtafaruku mkubwa.
Katika
mtafaruku huo ilpelekea vijana kuuchukua mwili wa marehemu hadi kwenye makaburi
huku wakimwacha mchungaji ambapo ililazimu jeshi la polisi kuingilia kati na
kuzuia fujo kanisani na kuamua kumresha nyumbani kwake kwa ulinzi mkali.
Wakati
mchungaji akisindikizwa nyumbani kwake vijana waliendelea na taratibu za
mazishi kwa utaratibu uliosimamiwa na Mwenyekiti wa Bodaboda Jiji Vicent
Mwashoma huku mchungaji wa Bodaboda Bahati Mwasote akiendesha Ibada ya mazishi.
Katika
mazishi hayo baadhi ya Viongozi mbalimbali walishiriki akiwemo mlezi wao Nwaka
Mwakisu,Mlezi wa Bodaboda Taifa Respisius Timanywa ambaye aliwaasa vijana
kuhudhuria mafunzo ili kupunguza ajali za mara kwa mara.
Kwa upande
wake mchungaji Edward Mtweve wa Kanisa la TAG amesema amesikitishwa sana na
kitendo cha kuvurugwa kwa Ibada kwani amesema kuwa wengi wa waliokuwa wakifanya
fujo walikuwa ni walevi na wavuta bangi na si waumini wa Kanisa lake.
Aidha Mtweve
na Baraza la wazee wamesema kuwa hawakusudii kuchukua hatua zozote dhidi ya
vijana ambao wamefanya fujo kwani yote wanamwachia Mungu na kwamba katika
kanisa hilo hakuna tukio lilowahi kutukia.
Pia amesema
kitendo cha kuchukua mwili wa marehemu madhabahuni ni cha utovu wa nidhamu
kwani vijana wanapaswa kuwa na hofu ya Mungu.
Wakikabidhi
rambirambi kwa mjane ,Mwenyekiti wa Bodaboda Jiji Vicent Mwashoma amesema pesa
za rambirambi zitumike kusaidia familia ya marehemu badala ya ndugu kutumia
pesa hizo kuendeshea msiba huo.
Na Ezekia Kamanga
Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment