Wasanii wakitoa burudani mbali mbali wakati wa sherehe za uzinduzi wa Chama hicho
WASANII wa maigizo na ngoma za asili
wametakiwa kuacha tabia ya kuiga tamaduni za nchi za nje na kuzifanyia kazi
badala ya kuenzi utamaduni wa Nchi yao kupitia sanaa wanazizifanya.
Mwito huo ulitolewa na Kaimu Mkuu wa
Mkoa wa Mbeya, Dk. Norman Sigalla ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, wakati
wa uzinduzi wa Chama cha Sanaa Jiji la Mbeya(CHASAMBE) uliofanyika katika
Viwanja vya chuo cha Uhasibu (TIA) Jijini hapa.
Sigalla alisema sanaa ni kitu pekee
kinachoweza kuchangia kudumisha utamaduni wa nchi yoyote kupitia michezo ya
kuigiza, kucheza ngoma, uchoraji, ufumaji, uhunzi na ufinyanzi kwa Msanii kuiga
vitu vilivyofanyika zamani kwa manufaa ya viziza vijavyo.
Alisema sanaa husaidia kujenga misingi
ya watu kufuata misingi na weledi wa utii wa sheria kutokana na wengi wao kuwa
katika vikundi mbali mbali hali inayosaidia kuhamasishana kwa manufaa ya taifa
jambo ambalo litachangia kuinua dira ya Mtanzania.
Aliongeza kuwa kitendo cha baadhi ya
wasanii kuiga utamaduni wa wazungu ni kupoteza maana ya sanaa na kuharibu
kabisa utamaduni wa Mtanzania kutokana na watu wanavyotazama kazi za wasanii
kwa wingi.
Sigalla alisema kupitia sanaa wananchi
wengi hupata ajira kutokana na kazi ya sanaa kutojali umri ambapo Watoto,
Vijana na Wazee hujumuika kwa pamoja hivyo husaidia hata kuondoa dhana ya kuwa
sanaa ni uhuni.
Kwa upande wake Mlezi wa Chama hicho
Jiji la Mbeya, Edna Mwaigomole alisema kazi ya malezi kwa vijana inapaswa
kufanywa ni kila mzazi bila kujali nafasi anayokuwa nayo kutokana na umuhimu wa
vijana kwa maendeleo ya Taifa.
Naye Mwenyekiti wa Chama hicho, Samweli
Mwamboma alisema madhumuni ya kuanzisha chama na kukizindua rasmi ni kutetea
maslahi ya wasanii wa sanaa zote.
Aliongeza kuwa madhumuni mengine ni
kuhamasisha unndwaji wa vikundi vingi vya sanaa ndani ya jiji la Mbeya, kuleta
umoja na mshikamano miongoni mwa wasanii na kuhamasisha wasanii sanaa
kama kazi ya kuwaingizia kipato. kuipenda
Mwenyekiti huyo alisema changamoto kubwa
inayowakabili wasanii wa Jiji la Mbeya ni kukosa motisha kutoka kwa baadhi ya
wadau ikiwa ni pamoja na serikali kushindwa kuwajengea uwezo kutokana na
kuwaita katika shughuli za Kiserikali na kutoa fedha kidogo isiyoweza
kukidhi haja.
Alisema mara nyingi Serikali haiangalii
kikundi kinawatu wangapi ambapo baada ya kufanya kazi ya kutoa burudani katika
sherehe huambulia malipo ya kati ya Shilingi 30,000 hadi 50,000 wakati kikundi
kinakuwa na watu kati ya 15 hadi 40.
Hata hivyo Katibu wa CHASAMBE, Bahati
Shulula alisema kutokana na changamoto zinazowakabili wasanii wa Mkoa wa Mbeya
kunaongeza kasi ya wasanii wengi kukimbilia Jijini Dar Es Salaam kwa kuamini
kuwa fursa nyingi zinapatikana huko.
Alisema Vijana wanafikiri fursa
zinazopatikana Dar haziwezi kufika mikoani kama makongamano ya Vijana
kutoandaliwa mikoani, kitendo cha Raisi Kikwete kuongea na Wasanii walioko Dar
bila kupata wawakilishi kutoka miko yote kinahamasisha kukimbilia huko.
Na Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment