Wakazi wa Mwakibete wakishuhudia kuchomwa kwa kamba hiyo
Imani za
kishirikna zimezidi kuchukua sura mpya mkoani Mbeya baada ya mwanamke
aliyefahamika kwa jina la Lucy Frank[55]mkazi wa Manyoni Singida kudai kamba
iliyotumika kushushia jeneza la marehemu dada yake apewe ili aende nayo
Singida.
Kauli hiyo
aliitoa katika msiba wa marehemu dada yake aliyefahamika kwa jina la Elizabeth
Sibonike[81] aliyefariki ghafla Novemba 19 mwaka huu katika mtaa wa Viwandani
kata ya Mwakibete na mazishi yake kufanyika Novemba 21 mwaka huu.
Baada ya
mazishi Lucy alidai dada yake kuwa kadhalilishwa kwa kuzikwa kwenye jeneza
kubwa na kushushwa kaburini kwa kutumia kamba aina ya manila,akidai vijana
walimtuhumu marehemu kuwa ni mshirikina hali iliyomkasirisha.
Katika hali
isiyokuwa ya kawaida mwanamke Lucy Frank alitamka msibani kuwa yeyote aligusa
kamba makaburini atakufa hali ambayo iliwaudhi wakazi wa mtaa huo na kumtaka
mwenyekiti wa mtaa Bwana Ndongole Mwatebele kuichukua kamba hiyo na kuitisha
mkutano wa hadhara ili mwanamke huyo kutoka Manyoni aeleze umma sababu za
kitaka kamba hiyo.
Hata hivyo
wananchi wa mtaa wa Viwandani wakitafakari hayo kijana mmoja miongoni mwa
waliokamata kamba makaburini
aitwaye Julius Mwandambo alifariki kwa kugongwa na gari eneo la mama
John Desemba 15 mwaka huu hali iliyowafanya wananchi kutaharuki.
Wakati
taratibu za mazishi zikiendelea Desemba 16 wakati picha ya marehemu ikitembezwa
barabarani mtoto wa Lucy alisikika akisema kama aliyefariki ni huyu, bado
wengine watafuata hali iliyowafanya vijana kugoma kuchimba kaburi mpaka atafutwe
huyo mama na mwanae ili waeleze kauli zao zina mantiki gani.
Katika hali
hiyo ya mtafaruku mama huyo na mwanae walienda kuhojiwa kituo cha Polisi kati
ambapo mtoto alikiri kutamka maneno hayo ingawa alisema kuwa hakujitambua hivyo
anaomba radhi.
Huku
wananchi wakimsubiria mwanamke huyo na mwanae kwenye mkutano ilidaiwa kutoroka
kwenda Singida na kwamba wananchi hawako tayari kuwaona warudi mtaani hapo.
Mkutano
ulioitishwa Desemba 27 mwaka huu ulioitishwa na viongozi mbalimbali wakiwemo
viongozi wa Muungano wa jamii Tanzania[MUJATA]akiwemo Soja Masoko,Abdul
Aziz,Diwani Kata ya Mwakibete Lucas Mwampiki na Chifu Shadrack Merere kutoka
Mbarali.
Chifu Merere
alitaka amani katika mtaa huo na kuamua kuiteketeza kamba kwa moto huku umati
ukishuhudia tukio hilo na chifu kuahidi kumrejesha kwa mazingara eneo la
Mwakibete ili ajibu tuhuma zinazomkabili
Na Ezekia Kamanga
Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment