Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Tuesday, October 1, 2013

Asasi isiyokuwa ya kiserikali ya APEC Imehitimisha mafunzo kwa madereva wa Bodaboda Wilaya ya CHUNYA yaliyojumuisha wahitimu wapatao 170 ambapo wamekabidhiwa vyeti na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya DIWANI ATHUMANI.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya akikaribishwa kuingia ukumbini na waendesha bodaboda
mkufunzi wa asasi ya APEC RESPIRIUS TIMINYWA amesema kuwa changamoto inayoikabili asasi yake ni kutojitokeza kwa madereva wa Bodaboda ili kupatiwa mafunzo licha ya kutumia nguvu kubwa kuhamasisha.
TIMINYWA ameiomba serikali kuipa asasi yake ruzuku ya mafuta ili iweze kuwafikia watu wengi na kutoa mafunzo ili madereva wapate uelewa na kupunguza ajali za barabarani ambazo nyingi husababishwa na uzembe
Kamanda wa Poilisi Mkoa wa Mbeya DIWANI ATHUMANI ameipongeza asasi ya APEC kwa kusaidia kutoa mafunzo kwa madereva wa Bodaboda kwani kwa kiasi kikubwa imesadia kupunguza ajali na pia Jeshi limepata mafanikio kupitia dhana Polisi Jamii na Ulinzi shirikishi.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya akimkabidhi cheti moja ya wahitimu




Asasi isiyokuwa ya kiserikali ya APEC Imehitimisha mafunzo kwa madereva wa Bodaboda Wilaya ya CHUNYA yaliyojumuisha wahitimu wapatao 170 ambapo wamekabidhiwa vyeti na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya DIWANI ATHUMANI.

Mafunzo hayo ya siku saba ambayo yalifunguliwa na Katibu Tawala wilaya ya CHUNYA SOSTEN MAYOKA ambaye amesema Mkuu wa wilaya DEODATUS KINAWIRO anaunga mkono juhudi za waendessha pikipiki kwa kuunda umoja ili kujikwamua kiuchumi.

KINAWIRO ameahidi kutoa shilingi laki tano kwa ajili ya kuimarisha kikundi hicho ili kuunda SACCOS ya waendesha BODABODA  na Halmashauri tjenga vituo viwili vya maegesho ya pikipiki eneo la MAKONGOLOSI na CHUNYA mjini ili kuondoa adha ya ukosefu wa vituo vya maegesho.

Kwa upande wake mkufunzi wa asasi ya APEC RESPIRIUS TIMINYWA amesema kuwa changamoto inayoikabili asasi yake ni kutojitokeza kwa madereva wa Bodaboda ili kupatiwa mafunzo licha ya kutumia nguvu kubwa kuhamasisha.
TIMINYWA ameiomba serikali kuipa asasi yake ruzuku ya mafuta ili iweze kuwafikia watu wengi na kutoa mafunzo ili madereva wapate uelewa na kupunguza ajali za barabarani ambazo nyingi husababishwa na uzembe.

Kwa upande wake Kamanda wa Poilisi Mkoa wa Mbeya DIWANI ATHUMANI ameipongeza asasi ya APEC kwa kusaidia kutoa mafunzo kwa madereva wa Bodaboda kwani kwa kiasi kikubwa imesadia kupunguza ajali na pia Jeshi limepata mafanikio kupitia dhana Polisi Jamii na Ulinzi shirikishi.

Aidha DIWANI amewaasa wahitimu kuwa makini  katika kazi zao ili kuepukana na wizi wa pikipiki na mauaji kwa kutobeba abiria zaidi ya mmoja kwani kufanya hivyo wanajihatarishia maisha yao lakini pia wayatumie mafunzo hayo ili kuleta ueledi wawapo barabarani.

Mafunzo hayo pia yanafanyika pia MKWAJUNI ambapo yamefunguliwa na Diwani wa Kata ya MKWAJUNI Mheshimiwa CHESCO NGAIRO Ambaye aliwataka madereva wa bodaboda kujitokeza kwa wingi ili kupata mafunzo hayo ambapo yatahitimishwa SEPTEMBA 3 mwaka huu.

Na Mbeya yetu

No comments: