Mashabiki wakishangili ushindi uwanjani hapo
Timu ya mpira wa Pete ya Filbert Bayi ya Kutoka
Dar Es Salaam imefanikiwa kunyakua ubingwa wa Ligi daraja la Kwanza msimu wa
2013 kwa mara ya pili mfululizo baada ya kuwachabanga wapinzani wao kwa
bila huruma.
Timu hiyo imefanikiwa kuchukua ubingwa katika
ligi iliyoanza Agosti 28, Mwaka huu na kukamilika Septemba Mosi, Mwaka huu na
kuzikutanisha timu za Netboli 12 kutoka maeneo mbali mbali, ligi iliyokuwa
ikifanyika katika uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine Mkoani Mbeya.
Timu ya Filbert Bayi ambayo mchezo wa Mwisho
ilicheza na timu ya Jkt Mbweni katika mchezo uliokuwa na upinzani mkali ambapo
Filibert Bayi walifanikiwa kuondoka na pointi zote baada ya kuwachabanga
wapinzani wao kwa jumla ya magoli 22 kwa 21.
Hadi mwisho wa Ligi hiyotimu ya Filbert Bayi
ilikuwa ikiiongoza ligi ikiwa na alama 22 huku ikiwa imecheza michezo 11 na
kufunga magoli 391 huku ikiruhusu magoli 181 katika lango lao kutoka katika timu zote.
Akitangaza msimamo wa ligi hiyo katika fainali
zilizofanyika katika Uwanja wa Sokoine na kufungwa na Naibu Waziri wa Elimu na
Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo, Katibu wa Chaneta Taifa, Maimuna Mrisha
amesema timu zote zilikuwa na upinzani mkubwa hali inayoonesha maandalizi
yalikuwa maziri.
Naye Katibu wa Chaneta Mkoa wa Mbeya, Pudensiana
Baitu amaesema michuano ya mwaka huu ilikuwa inakabiliwa na changamoto ya
fedhaambayo imesababishwa na makampuni kutokuwa wazi pindi wanapoombwa
michango.
Amesema bajeti ya michuano hiyo ilikuwa Milioni
16,400,000 lakini fedha amazo zilikuwa zimekusanywa zilifikia Milioni 2,500,000
hadi ligi inaisha hivyo kubakiza deni la shilingi Milioni 1,200,000.
Aidha kufuatia uwepo wa deni hilo Katibu huyo
amesema wamejitahidi kujibana lakini fedha hiyo ilitakiwa kulipia malazi kwa
viongozi wa Chaneta taifa ambapo deni hilo lililipwa papo hapo baada ya
Mc wa shughuli ya ufungaji Charles Mwakipesile kuchangisha fedha hizo kutoka
kwa wageni waliohudhuria ambalo lilipwa na Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya Musa Zungiza,
Mkurugenzi wa Filbert Bayi, Afisa Uhamiajiwa Mkoa wa Mbeya na Mwakipesile.
Mwenyeki wa Chaneta Taifa, Annah Kibira alitangaza kuwa timu zote
zilizoshiriki ligi daraja la kwanza msimu huu hakuna timu itakayoshuka daraja
hivyo zote zitaendelea kubaki ligi daraja la kwanza.
Na huu ndiyo msimamo wa ligi hiyo.
TIMU
|
IDADI YA MICHEZO
|
MAGOLI ALIYOFUNGA
|
MAGOLI ALIYOFUNGWA
|
ALAMA
|
Filbert Bay
|
11
|
391
|
181
|
22
|
JKT Mbweni
|
11
|
401
|
185
|
20
|
Magereza Morogoro
|
11
|
352
|
249
|
17
|
Jeshi Star
|
11
|
311
|
217
|
17
|
Hamambe
|
11
|
332
|
299
|
13
|
Uhamiaji
|
11
|
283
|
258
|
13
|
JKT Ruvu
|
11
|
280
|
309
|
9
|
Polisi Arusha
|
11
|
196
|
272
|
8
|
TTPL Morogoro
|
11
|
258
|
322
|
7
|
Polisi Mwanza
|
11
|
243
|
316
|
4
|
Polisi Mbeya
|
11
|
166
|
376
|
2
|
CMTU Dsm
|
11
|
185
|
365
|
0
|
Na Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment