Wafanyakazi wa Shirika la Taifa wa
Hifadhi ya Jamii (Nssf) Mkoa wa Mbeya wametoa msaada wa vyakula kwa watoto
yatima na waishio katika mazingira magumu eneo la Soko matola Jijini Mbeya ili
waweze kusherekea sikukuu ya Iddi.
Msaada huo uliotolewa na wafanyakazi
hao wa NSSF ni Mchele kilogramu 160, mafuta ya kupikia plastiki moja, Chumvu
katoni moja na Mbuzi wawili.
Watoto hao wapatao 30 wamekusanywa
na viongozi wa dini ya kiislamu katika madrasa ya Ittihal iliyopo eneo hilo
la Soko matola.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi
msaada huo wa vyakula vyenye thamani ya shilingi laki sita, Meneja wa Nssf Mkoa
wa Mbeya, Robert Kadege, alisema wafanyakazi wa shirika hilo maeneo mbalimbali
wamekuwa na utamaduni wa kujichangia na kuisadia jamii isiyojiweza wakiwemo
watoto waishio katika mazingira magumu.
Alisema wamekuwa wakiguswa
wanaposikia ama kuaona watoto yatima wakiwa wanaranda randa mitaani baada ya
kuwakosa wazazi ama walezi.
“Sisi wafanyakazi wa nssf tumekuwa
na utamaduni wetu katika kuisadia jamii wakiwemo watoto, hivyo baada ya kupata
tarifa kwa kituo hiki kimewakusanya watoto toka maeneo mbalimbali tumeamua
kujichanga chochote na kuwaletea ili waweze kupata chakula kwa ajili ya sikukuu
ya Idd” alisema Meneja huyo.
Aidha, Meneja huyo alisema jitihada
zinazowafanywa na viongozi wa madrasa hiyo katika kuwapatia watoto hao elimu ni
jambo la msingi kwani lengo lake ni kuondakana na taifa lenye watu mbumbuu.
Kwa upande wake heckh wa Madrasa hiyo, Sheickh Abbas Mshauri, alisema kuwa licha ya wao kuwa wanafundisha
masuala ya kiislamu lakini pia kimeamua kuwakusanya watoto wote bila kujali
itikadi ya kidini lengo ni kuona wanapata msaada wa karibu kutoka kwa wadau.
“Tunashukuru sana kwa msaada wenu
utakaotuwezesha kuwapatia watoto hawa kwenye sherehe ya Idd” alisema Sheickh
huyo.
|
No comments:
Post a Comment