Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Monday, August 5, 2013

TEMBELEA BANDA LA RAPHAEL GROUP LIMITED KATIKA MAONESHO YA NANE NANE MBEYA

MAMBO  MBALIMBALI  WANAYOFANYA RAPHAEL   GROUP LIMITED WASINDIKAJI WA MCHELE UYOLE MBEYA 
HILI NDILO BANDA LA RAPHAEL  GROUP  MACHINES 

MENEJA WA UZALISHAJI WA RAPHAEL MACHINES GROUP LTD, PETER D. MLEGULAH AKITOA MAELEZO YA KINA YA JINSI WANAVYOFANYA KAZI ZAO 

WATUMISHI WA RAPHAEL GROUP LIMITED, KUTOKA KUSHOTO NI CHRISTOPHER MBILINYI (MUUZAJI), LAZARO MWAKIPESILE (KITENGO CHA MASOKO), PETER MLEGULAH(MENEJA WA UZALISHAJI), LUCY MWAKALAMBILE(MUUZAJI), MAMA  MUSYANI(MUHASIBU) 

EZEKIA WILSON(KITENGO CHA MASOKO) AKIONESHA MOJA YA BIDHAA ZA RAPHAEL GROUP 
 MCHELE AINA YA BROWN RICE AMBAO NI MAALUM KWA AJILI YA WATU WENYE KISUKARI AMBAO KILO MOJA INAUZWA TSH . 2000 TU
 KUSHOTO NI MCHELE WA KYELA GRADE 1 NA KULIA NI MCHELE WA KAMSAMBA GRADE 1 YOTE INAUZWA TSH 1500 KWA KILO MOJA 
 HII NI PUMBA  KWA AJILI YA MIFUGO PAMOJA NA KUTENGENEZEA NISHATI YA UMEME KILO MOJA INAUZWA TSH 50 

 KUSHOTO NI MCHELE WA KYELA KG 20 UNAOUZWA TSH 30,000 NA UPANDE WA KULIA NI MCHELE WA KYELA KG 10 UNAUZWA TSH 15,000
KARANGA NYEKUNDU NA NYEUPE ZINAZOINGIZWA NCHINI NA KUUZWA NA RAPHAEL GROUP LIMITED ZIKITOKEA MALAWI KWA KILO MOJA NI TSH 2000

*******
WITO umetolewa kwa serikali kuhakikisha inakuwa karibu na Sekta binafsi ambazo zimekuwa zikijishughulisha hasa na  kazi kuwainua wakulima wadogo ili kuhakikisha wanafikia malengo yao.

Akizungumza katika viwanja vya maonyesho ya Nanenane vya John Mwakangale jijini Mbeya Meneja wa Kampuni ya Raphael Group Machines   Ndugu  Peter Mlegulah waliopo Uyole jijini hapa  amesema kuwa nivema serikali sasa akizitambua sekta binafsi katika kukuza uchumi wa Taifa .

Amesema katika Kampuni yake ambayo inahusika zaidi na shughuli za kilimo hasa usindikaji wa mazao  kwa sasa imeweza kuwasaidia wakulima zaidi ya elfu 4 ambao wameweza kupata elimu pamoja na kukopeshwa pembejeo za Kilimo.

Amesema toka waanze shughuli hiyo wana miaka zaidi ya 15 ambapo kazi kubwa waliyonayo ni pamoja usindikaji wa bidhaa za Michele pamoja zao la karanga pamoja na kuwasaidia wakulima wadogo ili waweze kufikia malengo yao hasa kwa kuwapatia elimu ya kilimo na ushauriwa kitaalam.

Amesema wakulima walio wawezesha wameweza kuondokana na kilimo cha kienyeji ambapo kwa sasa wakulima hao wameweza kuinuka kwa kuongeza uzalishaji toka gunia 40 hadi gunia 80 kwa Hekta, hivyo kampuni hiyo imekuwa mkombozi  mkubwa kwa wakulima wa Kanda ya Nyanda za juu kusini.


Amesema malengo yao ni kuwafikia wakulima zaidi ya Laki moja(100,000) ili kuhakikisha wanaisadia serikali katika kupunguza tatizo la ajira nchini kwa kudhibiti idadi kubwa ya vijana wanao toka vijijini na kukimbilia mijini.

WASILIANA  NAO SASA KUPTIA SIMU NAMBA +255 784 409340 NA  +255 767 409340 

TEMBELEA WEBSITE YAO: www.rafagrouplimited.com

1 comment:

judith said...

kazi nzuri mpaka raha