MNAMO
TAREHE 22.08.2013 MAJIRA YA
SAA 00:30 HRS HUKO KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA KYELA
MKOA WA MBEYA. ARON S/O MSOLE, MIAKA
70, MNDALI, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA IBANDA ALIFARIKI DUNIA WAKATI
AKIENDELEA KUPATIWA MATIBABU HOSPITALINI HAPO. CHANZO NI BAADA YA KUPIGWA JIWE UBAVUNI NA ANANIA S/O SIMTOE, MIAKA 50,
MNYAMWANGA, MKULIMA, MKAZI WA IBANDA KUFUATIA NG’OMBE WAKE KUINGIA KATIKA
SHAMBA LA MAREHEMU NA KUHARIBU MAZAO. MWILI WA MAREHEMU UMEFANYIWA UCHUNGUZI NA
DAKTARI WA SERIKALI NA KUKABIDHIWA NDUGU KWA MAZISHI. MTUHUMIWA AMEKAMATWA.
TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUTATUA
MATATIZO/MIGOGORO YAO KWA NJIA YA
KUKAA MEZA YA MAZUNGUMZO
ILI KUEPUKA MATATIZO YANAYOWEZA KUEPUKIKA.
WILAYA
YA MOMBA – AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU NA
KUSABABISHA KIFO.
MNAMO
TAREHE 22.08.2013 MAJIRA YA
SAA 05:30 HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA MPEMBA BARABARA YA
MBEYA/TUNDUMA WILAYA YA MOMBA MKOA WA MBEYA. GARI NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA JINA WALA
MAKAZI YAKE LILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU ASIYEFAHAMIKA
JINA WALA MAKAZI YAKE, JINSI
YA KIUME MWENYE UMRI KATI YA MIAKA 30-35 NA KUSABABISHA KIFO CHAKE
PAPO HAPO. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KITUO CHA AFYA TUNDUMA. DEREVA
ALIKIMBIA NA GARI MARA BAADA YA
TUKIO. . KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI
DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVAKUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO
KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA
KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA AZITOE KATIKA
MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE, VINGINEVYO
AJISALIMISHE MARA MOJA.
Signed
by:
(DIWANI ATUMANI – ACP)
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
No comments:
Post a Comment