Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Chrispin Meela akitoa Hotuba katika Msikiti Mkuu wa Mbeya kwa waumini wa Dini ya Kiislam wakati wa Baraza la Idd. |
Waumini Mbalimbali wa Dini ya Kiislam wakiwa katika Baraza la Idd
Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Chrispin Meela wa pili kutoka kushoto akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Dini ya Kiislam
Imeelezwa kwamba Serikali pamoja viongozi wa dini zote bado hawajampata adui anayevuruga amani ya nchi kwa misingi ya udini na Siasa.
Kauli hiyo
imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Mkoani Mbeya, Chrispin Meela, wakati
akiwahutubia waumini wa dini ya kiislamu kwenye baraza la Eid
iliyofanyika hivi karibuni katika msikiti mkuu wa Mkoa wa Mbeya.
Meela alisema kuwa
hivi sasa nchi inavurugwa kwa misingi ya Udini na Siasa huku wanaokamatana
uchawi wakiwa ni watanzania wenyewe bila ya kujua kiini cha mtu anayeanzisha
vurugu hizo.
Alidai kuwa hali
hiyo inawezekana kwamba kuna mkono wa mtu kutoka hata nje nchi anayetaka kuona
nchi inakuwa haina amani na si vingenevyo.
“Viongozi wa dini
zote, Serikali na viongozi wanasiasa ni lazima tukaye chini tutafakari kwa
kiina na kumtafuta mchawi anayetuvuruga badala ya kukamatana uchawi sisi
kwa sisi na hapa lazima kuna mkono wa mtu mwingine na isitoshe anatoka hata nje
ya nchi hasa tukirejea historia ya utamaduni wetu watanzania hatukwa na
mvurugano kama huu wa sasa kwa miaka mingi iweje leo hii,” alisema Meela.
Alisema hivi sasa
kinachofanyika kwa watanzania kulipizana visasi ambavyo hata havina ukweli
wowote kwani akipigwa mwislamu kauli inatolewa kwamba ni mkristo ndiye
aliyefanya hivyo na mkristo akipigwa eti mwislamu ndiye aliyehusika.
Hali kadharika
Meela, alisema hata kwenye masuala ya Siasa mtindo mmoja ambapo vurugu
zikitokea katika mkutano wa Chadema basi CCM ndio waliofanya vurugu hizo
ama zikitokea katika Mkutano wa CCM basi vivyo hivyo Chadema ndio chanzo.
Alisema kuwa bado
kuna kazi ngumu kwa viongozi wa dini na Serikali ya kumtafuta adui anayetaka
kuona nchi haitawaliki kwa misingi ya udini ama Siasa, huku mkuu huyo
wa Wilaya akiwasisitiza viongozi wa dini zote kuliombea taifa ili kuombana na
kasumba hiyo mbaya na inayoichafua sura ya nchi na watanzania wake.
No comments:
Post a Comment