Mbunge wa Jimbo la Rungwe Magharibi Profesa David Mwakyusa akizungumza na waumini wa kanisa la Wasabato wa Swebo Ntokela kuashiria ufunguzi wa harambee ya ujenzi wa kanisa. |
Watoto wakiingia kanisani kwa ukakamavu mkubwa kushiriki harambee hiyo. |
Mgeni rasmi Profesa Mwakyusa akiwa meza kuu pamoja na viongozi wa Kanisa la Sabato siku ya harambee. |
Kwaya ya Kanisa hilo ikitumbuiza kanisa hapo siku hiyo ya harambee. |
Katibu mkuu wa kanisa la Sabato Jimbo la Nyanda za juu kusini Mchungaji Steven Letter akisoma neno la Mungu kuashiria ufunguzi wa Harambee hiyo. |
Baadhi ya wageni waalikwa na waumini wakifuatilia kwa makini zoezi la Harambee lililokuwa likiendelea kanisani hapo. |
Katibu wa Kamati ya Maandalizi ya Harambee hiyo, Award Mpandilah na Jose Mwapamba wakisoma risala mbele ya mgeni rasmi. |
Award Mpandila akisimamia zoezi la uchangiaji wa harambee lilipokuwa likiendelea. |
Kamati ya maandalizi ya harambee hiyo ikiwa katika picha ya pamoja. |
Award Mpandila akimkabidhi hesabu ya jumla ya fedha zilizopatikana katika harambee hiyo Mgeni rasmi Profesa Mwakyusa. |
Mwonekano wa jengo la kanisa hilo lilipoishia na kulazimu kufanya harambee ili kumalizia ujenzi wake. |
Profesa
David Mwakyusa Waziri wa Afya wa Zamani na Mbunge wa sasa wa Jimbo la
Rungwe Magharibi(CCM) amefanikiwa kukusanya zaidi ya Shilingi Milion 40 katika
harambee ya uchangiaji ujenzi wa kanisa la Sabato la Swebo lililopo Ntokela
Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya.
Katika
Harambee hiyo Profesa Mwakyusa ambaye alikuwa Mgeni rasmi, kabla ya kuanza
kwa zoezi hilo aliwasihi waumini wa kanisa hilo kuacha tabia ya
kunung’unika pale wanapojitoa kwa ajili ya kusaidia shughuli mbali mbali za
kikanisa ambazo zinafanywa na makanisa hayo ili kusaidia jamii.
Imeelezwa
kuwa baadhi ya waumini wamekuwa na moyo wa kujitolea pindi misaada mbali mbali
inapohitajika katika makanisa, badala yake huanza kuumia katika mioyo yao
kwa kile walichotoa kwa kuona wametoa kiasi kingi.
Prof.
Mwakyusa alisema kama waumini wameamua kujitoa kwa ajili ya
shughuli za kanisa hawana budi kunung’unika ndani ya nafsi zao
kwani kazi ya mungu ni kujitolea si busara muumini kutoa msaada halafu ujutie
baadaye.
Akisoma
risala kwa mgeni rasmi mmoja wa wajumbe wa kamati ya maandalizi
ya harambee hiyo Bw.Awadi Mpandila alisema kuwa lengo la
kuanzisha ujenzi huo wa kanisa kulitokana na wingi wa waumini katika
kanisa hilo ambao wanafikia 835.
Award
alisema kuwa ujenzi huo ulianza mwaka 2002 na kiasi cha fedha
kilichotumika mpaka sasa ni mil.279 na zinazohitajika ili kuweza kukamilisha
jengo
hilo
ni sh. Mil.90.
Mbali
na kukamilika kwa Harambee hiyo Mpandila anatoa wito kwa wadau na marafiki wa
karibu ambao walipewa kadi za mwaliko lakini walikwama kufika kuendelea
kuchangia kutokana na fedha zilizopatikana kutokidhi kiwango.
Alisema
fedha hizo zinahitajika kwa ajili ya kupaua na kumalizia jengo la kanisa hilo
ambalo hatua za ujenzi wa awali umekamilika hivyo Wadau na marafiki
wamekumbushwa kumtolea Mungu kupitia ujenzi wa kanisa hilo.
Hata
hivyo katika harambee hiyo jumla ya sh. Mil.46 zilipatikana huku fedha
iliyochangwa papo kwa papo ni sh. Mil.23 huku ahadi zikiwa mil.23 .
Aidha katika harambee hiyo ,Prof. Mwakyusa
alichangia zaidi ya mil.2 pamoja na familia yake.
Na Mbeya yetu
No comments:
Post a Comment