Naibu kamishna wa madini John Nayopa akihutubia wanakikundi cha jikomboe kushoto ni katibu tawala wilaya ya Chunya Sosten Mayoka kulia ni kamishna wa madini kanda ya Mbeya John Shija
Kikundi cha wachimbaji wadogo wa madini cha JIKOMBOE cha
SAZA Wilayani CHUNYA kimeiomba serikali kutatua mgogoro unaohusu mlima
ELIZABETH baina ya makampuni ya SHANTA na BAFEX uliodumu kwa miaka mitatu sasa.
Mwenyekiti wa kikundi cha JIKOMBOE ROBERT NSELU amelalamika maamuzi ya wizara ya madini
kuwapendelea wawekezaji.
Mgogoro huo umeshindwa kupatiwa ufumbuzi kutokana na
mkanganyiko uliofanywa na maafisa wa madini wilaya ya CHUNYA baada ya kupokea
maombi kutoka kikundi cha JIKOMBOE na kuridhia maombi yao kisha Wizara kuwapa
leseni.
Mara baada ya kupewa leseni ya kumiliki mlima ELIZABETH
kampuni ya BAFEX iliibuka na kudai kuwa hilo ni eneo lake kihalali na kuzua
mtafaruku ambao ulipelekea mara kadhaa kujadiliwa na Afisa madini kanda Bwana
JOHN SHIJA bila mafanikio.
SHIJA baada ya kushindwa kutatua mgogoro huo aliamua
kuupeleka wizarani ambapo mara kadhaa wizara wameujadili bila kupatiwa ufumbuzi
hali iliyopelekea wizara kumwagiza Naibu Kamishina wa Madini JOHN NAYOPA ili
atatue suala hilo.
NAYOPA baada ya kutembelea mlima ELIZABETH alibaini makosa
yaliyofanywa na maafisa madini kwa kutoa Hekta 71 badala ya 10 zinazotakiwa
kisheria na isitoshe mchora ramani kuonesha kuwa ombi la TUJIKOMBOE ni la mtu
mmoja aliyefahamika kwa jina la JOSEPH MAKERERE.
Mbali ya hilo NAYOPA Amesema mchoro unaonesha kuwa kiwanja
hicho kipo MBARALI badala ya SAZA CHUNYA kama kilivyoombwa na TUJIKOMBOE Hali
ambayo NAYOPA inaashiria kuwepo mazingira ya rushwa.
Kuokana na utata huo NAYOPA Ameamua kuupeleka mgogoro huo
kwa waziri wa madini ili aweze kutolea uamuzi ambao utakuwa hitimisho la
mgogoro huo.
Wakati huo huo Kamishina wa kanda Bwana JOHN SHIJA amewapa
fursa kikundi cha JIKOMBOE kuleta maombi ya ardhi ya kuchimba kwa vile wao ni
kikundi hivyo atawapa kipau mbele kuhakikisha wanapata lesni kwa wakati.
Picha na Ezekiel Kamanga
Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment