Kamanda wa wa Polisi Mkoani MBEYA DIWAN ATHUMAN Ametoa vyeti
kwa madereva wa pikipiki maarufu kama Bodaboda zaidi ya 151 wa Igurusi Wilaya
ya Mbarali.
Madereva hao walikabidhiwa vyeti hivyo baada ya kupatiwa
mafunzo ya alama za usalama barabarani kwa msaada wa shirika lisilo la
Kiserikali kwa kushirikiana na Kikosi cha usalama Barabarani Mkoani Mbeya.
Mbali ya kukabidhiwa vyeti pia Madereva hao walipatiwa
leseni za udereva ambapo Diwani Athumani aliwataka madereva hao kuwa makini
barabarani na kuzingatia sheria za usalama barabarani.
Aidha Kamanda Diwani aliwashukuru madereva wa Bodaboda kwa
ushirikiano na Jeshi la Polisi kwa kufichua vitendo vya uhalifu Mkoani Mbeya
ambapo wamekuwa wakitoa taarifa za siri na kupunguza uhalifu mkoani Mbeya.
Hata hivyo Diwani alitumia fursa hiyo kuwataka madereva kuwa
makini kwani kwa kipindi cha miezi sita madereva 38 wa bodaboda wamefariki
mkoani Mbeya na kusikitishwa na wingi wa ajali hizo za pikipiki kwani wengi wao
ni vijana na ni nguvu kazi ya Taifa.
Na Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment