Askari Polisi wakimrejesha rumande
Bosi Mmalawi Evance Mwale anayeshitakiwa kwa makosa ya Rushwa ya Ngono
|
ALIYEKUWA Meneja wa Kampuni ya Malawi Cargo
tawi la Mbeya Evason Mwale(49) raia wa nchi jirani ya Malawi, amefikishwa
katika Mahakama ya Wilaya ya Mbeya akituhumiwa kujihusisha na Rushwa ya Ngono.
Mwendesha mashtaka wa Serikali Basilius Namkambe
akisoma Mashtaka ya mtuhumiwa huyo mbele ya Hakimu mkazi wa mahakama hiyo
Gilbert Ndeuluo alisema Mtuhumiwa anashtakiwa kwa makosa mawili ambayo ni
Rushwa ya Ngono kinyume cha kifungu cha 25 cha Sheria ya kuzuia na kupambana na
Rushwa namba 11 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2007.
Namkambe alidai mahakamani hapo kuwa mtuhumiwa
anashtakiwa kwa kosa lingine la matumizi mabaya ya madaraka kinyume cha kifungu
cha 31 cha Sheria ya kuzuia na kupambana na Rushwa namba 11 iliyofanyiwa
marekebisho mwaka 2007.
Alisema mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo April
11, Mwaka huu katika Hoteli moja iliyopo Iyunga Jijini Mbeya
ambapo alikamatwa akitaka kujihusisha na rushwa ya Ngono na Mke wa Mfanyakazi
wake.
Kwa upande wake Hakimu Mkazi Ndeoruo aliahirisha
kesi hiyo hadi Julai 1, Mwaka huu kwa ajili ya kuanza kusikiliza ambapo pia
alisema Dhama iko wazi kwa Mtuhumiwa kuwa na wadhamini wawili wenye hati za
mali isiyohamishika yenye thamani ya Shilingi Milioni 10, Barua zinazotambuliwa
na mamlaka, ambapo pia mtuhumiwa anatakiwa kuacha hati zake za kusafiria
na kutoruhusiwa kutoka nje ya Jiji la Mbeya bila ruhusa ya mahakama.
Awali ilidaiwa kuwa Meneja huyo alitaka
kujihusisha na Rushwa na Mke wa Mfanyakazi wake wa nyumbani ambaye alimfukuza
kazi na baadaye alimtumia Mkewe ili amrudishe kazini baada ya kufanya naye
mapenzi.
Na Mbeya yetu
No comments:
Post a Comment