Wananchi
wa Kata ya Iyunga mtaa wa IKuti jijini mbeya wamelalamikia kitendo
uongozi wa jiji la mbeya kushindwa kuzuia hali ya uchafu katika eneo la soko la
Ikuti jijini
Licha ya kuwepo kwa shughuli za kimaendeleo hasa
soko na shughuli nyiingine hali imekuwa mbaya katika eneo la soko hilo kutokana
na kuwepo kwa mirundikano ya uchafu katika ya soko hilo.
Wakizungumza juu ya kuwepo kwa hali hiyo
wananchi wa maeneo hayo wamedai kuwa takataka zilizo jazana katika eneo hilo la
soko linahatarisha afya za wakazi wa eneo hilo kutokana kuwepo na huduma muhimu
kama soko ambako kunauzwa vyakula na mahitaji mengine.
Mmoja wa wakazi hao ndugu Janneth Mbukwa amesema
kuwa kwa muda mrefu sasa takataka hizo zimekuwepo eneo hilo licha ya
wafanyabiashara wa eneo hilo pamoja na baadhi ya wananchi kutoa taarifa sehemu
husika ili kulifanyia kazi suala hilo.
Amesema kuwa licha ya kuwepo kwa uchafu huo kwa muda
mrefu bado mawakala wa kutoza ushuru wamekuwa wakikusanya michango kama kawaida
Licha ya kuwepo kwa hali hiyo ambayo ni adha kubwa kwa wakazi wa maeneo
hayo.
Amesema tatizo kubwa lililopo katika eneo hilo ni harufu
mbaya inayo toka eneo hilo ambapo kwa asilimia kubwa huathiri shughuli
zilizopo katika eneo hilo ambapo zaidi ya vibanda 20 vya mama ntilie vipo
eneo hilo la ghuba la taka hali ambayo imefanya wateja wao kuwa na hofu
juu ya afya zao.
|
No comments:
Post a Comment