Mwamwaja.
USAILI wa wagombea wanaowania
nafasi mbalimbali za uongozi katika chama cha soka mkoa
wa Mbeya, (MREFA), umegubikwa na vituko vya aina yake, baada ya mmoja wa
wagombea wa nafasi ya Uenyekiti, kumkataa mjumbe wa kamati ya uchaguzi
kwa madai kuwa ana mgongano wa kimasilahi na mpinzani wake.
Mjumbe wa Kamati ya uchaguzi
aliyekataliwa na kulazimika kutolewa ndani ya chumba cha usaili ili haki
itendeke kwa mgombea ni Katibu, Prince Mwaihojo, ambaye anadaiwa kuwa ni Mkwe
wa mgombea mmoja wa nafasi ya Uenyekiti John Mwamwaja.
Katibu huyo wa Kamati ya uchaguzi,
akitoka nje muda mfupi tu baada ya mmoja wa wagombea ya nafasi ya uenyekiti
Elias Mwanjala, alipoitwa ndani ya chumba cha usaili.
Kwa upande wake, Mwaihojo
alipoulizwa juu ya sakata hilo la kukataliwa, amekiri kuwa lilitokea na
si la ajabu katika mahala popote ambapo haki inafuatwa, hivyo kitendo hicho
hakizuii mchakato wa kuwapata viongozi wa chama hicho.
Akitoa taarifa ya mchakato wa
zoezi hilo baada ya kumalizika, Mwaihojo alisema zoezi hilo la usaili kwa
limefanikiwa kwa asilimia 90 kwa kuwa wagombea 14 walifanyiwa usaili na
kubakiza wagombea wanne tu ambao watamalizia hawakufanyiwa.
Kwa mujibu wa Mwaihojo,
wagombea wanne ambao hawajafanyiwa usali ni Katibu anayemaliza muda wake
Lawrence Mwakitalu, Andongwisye Panja, Thomas Kasombwe Sinkwembe ambao wote
walitoa udhulu kutokana na kukabiliwa na shughuli mbalimbali ikiwemo kusimamia
mitihani ya kidato cha nne inayoendelea hivi sasa.
Uchaguzi wa MREFA unatarajia
kufanyika oktoba 27, jambo litakalowezesha kupatikana kwa uongozi mpya
utakaohudumu kwa miaka mine kama katiba ya chama hicho inavyoeleza.
Aliwataja watu waliojitokeza kuomba
nafasi za uongozi kwa nafasi ya Mwenyekiti kuwa ni John Mwamwaja ambaye
ni makamu Mwenyekiti wa uongozi unaomaliza muda wake, wakati wengine ni Majuto
Mbuguyo aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji katika Halmashauri ya
Pamoja na Elias Mwanjala ambaye
katika uchaguzi Mkuu uliopita aligombea ubunge katika jimbo la Kyela na
kuangushwa vibaya na mbunge wa sasa Dk. Harrison Mwakyembe, ambaye pia ni
Waziri wa Uchukuzi.
Makamu Mwenyekiti ni Omary
Mahinya, wakati nafasi ya Katibu Mkuu, Lawrence Mwakitalu, anayemaliza muda
wake,Suleiman Haroub na Redson Kaisi, ambapo Katibu Msaidizi ni William
Mwamlima na nafasi ya Mkutano Mkuu wa Taifa Tahdeo Kalua na Danny Korosso.
Kwa upande mweka Hazina ni Asajile Kavenga,
Uswege Luhanga, wakati wajumbe wa kamati ya utendaji ni Lwitiko Mwamndela,
Thomas Kasombwe, Boniface Sinkwembe.
kwa hisani ya Moses Ng’wat, Mbeya
No comments:
Post a Comment