KIKUNDI cha huduma za majumbani Mkoani Mbeya (KIHUMBE) kimesema kuwa bado kina changamoto kubwa kutoka kwa jamii wakati wa kutoa huduma hizo ambapo baadhi ya familia pale zinapopewa misaada huuza na wazazi wengine kudanganya kuwa watoto wao ni yatima ili wapatiwe misaada.
Mwandishi wetu Esther Macha anaripoti kutoka Mbeya kuwa akizungumza na mtandao huu ofisini kwake Meneja wa shirika hilo Bw. Bw.Ptolemy Samweli alisema kuwa kati ya vitu ambavyo vinawapa wakati mgumu katika shirika hiloi ni pamoja na changamoto hizo za kutoonyesha uaminifu wakati wa utoaji wa misaada.
“Sisi tunalenga zaidi watoto yatima lakini kitendo cha wazazi kuongea uongo ni kitu kibaya sana wakati kuna familia ni maskini kabisa kwanini sisisaidiwe kwanza hizo,hawa wanaokuja kudanganya unakuta wazazi wao wapo na wanaokuja kusema ni wazazi wenyewe kuwa watoto hao ni yatima ,tunaomba wazazi wawe na huruma kwani hata hawa walio yatima hawakupenda”alisema.
Alisema kuwa wangependa kusaidia na jamii zingine lakini lengo ni kusaidia kwanza yatima ambao hauna mwelekeo wowote wa kimaisha, na fedha wanazopewa ni kidogo na wadhadhili ambazo zimelengwa kwa watu maalumu tu.
Akizungumzia kuhusu magodoro ambayo wamekuwa wakipewa na shirika hilo Bw. Samweli alisema kuwa baadhi ya familia zimekuwa zikidiriki kuuza ili waweze kupata fedha kitu ambacho si kizuri.
“Si jambo jema kwani mtu unapopewa msaada ili ukusaidia hutakiwi kuuza, hata kama una matatizo yako basi tafuta nyingine ya kutatua lakini si kuuza kwani kama shirika tunapojaribu kutoa misaada hiyo kwa jamii hizi tunaweka usawa Fulani wa maisha kwao”alisema Meneja huyo.
Aidha Meneja huyo alisema wagonjwa wengine kuacha dawa na kuipa hasara serikali na kwamba kwani baada ya kuacha ugonjwa huo hurudi kwa kasi kubwa.
Akizungumzia jinsi ya kuwatambua watoto yatima Bw.Samweli alisema katika halmashauri ya Jiji la Mbeya kuna program maalumu ya ya kuwatambua watoto yatima ambayo ipo Ustawi wa Jamii ambapo wao kama shirika hufika na kuwachukua hapo ambao tayari wanakuwa wamehakikiwa na serikali ya Mkoa.
Alisema katika kufanya hivyo ndo wanakuwa wamepata uhakika kuwa wamepata watoto hao licha ya kuwa bado kunakuwa na mahitaji makubwa ya watoto kuhitaji kuhudumiwa na shirika,lakini bado uwezo mdogo kama watoto wanachukuliwa inabidi wapewe huduma zote kulingana na mahitaji.
No comments:
Post a Comment