Muuguzi kutoka Hospitali Teule ya Ifisi iliyopo mji mdogo wa Mbalizi wilaya ya Mbeya vijijini Bi Tabu Kumwenda, akiufanyia uchunguzi mwili wa marehemu Ndele Shantiwa (30), aliyeuawa kwa kukatwakatwa kwa mapanga na shoka na wananchi wenye hasira baada ya kushirikiana na wenzake wawili ambao ni Ndele Rujewa na Mboya kuiba mali zenye thamani ya shilingi 586,000/= za kitanzania mali ya Bwana Geofrey Kabiba
Mguu wa kulia ukiwa umekatwa kwa Panga ambao ni wa marehemu Ndele Shantiwa (30), aliyeuawa kwa kukatwakatwa kwa mapanga na shoka na wananchi wenye hasira baada ya kushirikiana na wenzake wawili ambao ni Ndele Rujewa na Mboya kuiba mali zenye thamani ya shilingi 586,000/= za kitanzania mali ya Bwana Geofrey Kabiba
Marehemu Ndele Shantiwa (30), akiwa amefungwa kwenye mti, amapo ameuwawa kuawa kwa kukatwakatwa kwa mapanga na shoka na wananchi wenye hasira baada ya kushirikiana na wenzake wawili ambao ni Ndele Rujewa na Mboya kuiba mali zenye thamani ya shilingi 586,000/= za kitanzania mali ya Bwana Geofrey Kabiba.
*****
Na Mwandishi wetu Ezekiel Kamanga
Na Mwandishi wetu Ezekiel Kamanga
Watu wawili wameuawa mkoani Mbeya katika matukio mawili tofauti yanayohisishwa na wizi likiwemo la Ndele Shantiwa mwenye umri wa miaka 30, aliyeuwawa kwa kukatwakatwa na mapanga na shoka jana na wananchi wenye hasira kali majira ya saa nne asubuhi katika kijiji cha Njelenje, kata ya Mshewe wilaya ya Mbeya vijijini mkoani Mbeya.
Marehemu Ndele amekatwakatwa sehemu mbalimbali za mwili wake, ikiwemo kiwiko cha mguu wake wa kulia(kuume) na mkono wa kushoto hali iliyopelea kuvuja damu nyingi ambapo wananchi hao kabla ya kumuua walimfunga mikono na miguu katika mti na kuanza kumwadhibu hadi kifo chake.
Ndele akiwa na wenzake wawili wanaofahamika kwa majina ya Ndele Rujewa na Mboya inadaiwa majira ya saa 7 usiku walivunja na kuiba sukari katoni 1 yenye thamani ya shilingi 44,000, Inveta yenye thamani ya shilingi 150,000, sabuni katoni 1 yenye thamani ya shilingi 20,000, chumvi katoni 1 sawa na shilingi 12,000, mchele debe 2 zenye thamani ya shilingi 80,000, vitenge doti 2 sawa na shilingi 42,000, kandambili jozi 12 thamani ya shilingi 130,000 ambapo mali yote ilikuwa na thamani ya shilingi 586,000.
Hata hivyo watu wawili walinusurika kuuwawa na wananchi hao wenye hasira kali baada ya kufanya jitihada za kutaka kumwokea Ndele Shantiwa kwa kuzuia wananchi wasimpige ambapo ni Angumbwike Mwaikuyu na Wiliam Kameme.
Mwenye kiti wa kitongoji Bwana Mbuwa Khamis ametibitisha kutokea kwa tukio hilo la mauaji ambapo alitoa taarifa kwa Jeshi la polisi ambao walifika eneo la tukio wakiwa na Muuguzi wa Hospitali ya Ifisi Bi Tabu Kumwenda ambaye aliufanyia uchunguzi mwili wa marehemu, na mara baada ya uchunguzi kukamilika mwili wa marehemu ulikabidhiwa kwa kaka wa marehemu Bwana Jackson Shantiwa(45) kwa ajili ya mazishi.
Tukio la pili limetokea katika kijiji cha Mkanga wilayani Mbozi ambapo Hatibu Kibasi(36), ameuawa baada ya kupingwa na wananchi wenye hasira kali baada ya kuiba akiwa mnadani.
Kamanda wa polisi mkoani Mbeya Advocate Nyombi amethibitisha kutokea kwa matukio hayo na kamba jeshi la polisi linafanya uchunguzi ili kuweza kubaini waliohusika na matukio hayo na kwamba mharifu anapokamatwa afikishwe kwenye vyombo vya sheria ili kujibu tuhuma zinazomkabili na sio wananchi kujichukulia sheria mkononi.
No comments:
Post a Comment