Vyombo na samani za aliyekuwa Mwenyekiti wa mtaa wa Igoma A, kata ya Isanga jijini Mbeya Bwana Juma Kahawa vilitolewa nje hapo jana kabla ya wananchi wa Igoma B nyumbani kwa dada yake Bi Mary James mwenye umri wa miaka 50 ambaye pia ni balozi wa mtaa huo, ambako Bwana Kahawa amehamia ndipo wananchi wa mtaa huo kuamua kuviteketeza kwa moto kwa madai kuwa hawamtaki Bwana Kahawa kuhamia mtaani kwao kutokana na kujihusisha na imani za kishrikina.
Umati wa wananchi wa mtaa wa Igoma B kata ya Isanga jijini Mbeya uliofika kushuhudia uteketezwaji wa vyombo na samani za aliyekuwa Mwenyekiti wa mtaa wa Igoma A, Bwana Juma Kahawa ambaye amehamia nyumbani kwa dada yake Bi Mary James mwenye umri wa miaka 50 ambaye pia ni balozi wa mtaa huo, ndipo wananchi wa mtaa wa Igoma B kuamua kuviteketeza kwa moto kwa madai kuwa hawamtaki Bwana Kahawa kuhamia mtaani kwao kutokana na kujihusisha na imani za kishrikina.
Balozi wa mtaa wa Igoma B, kata ya Isanga jijini Mbeya Bi Mary James ahamini kilichotokea baada ya samani zikiwemo zake na za kaka yake Bwana Juma Kahawa kutolewa nje na kuteketezwa kwa moto na wananchi wa mtaa huo kutokana na madai kuwa hawamtaki Bwana Kahawa aliyekuwa Mwenyekiti wa mtaa ya Igoma A anayetuhumiwa kujihusisha na imani za kishirikina.
Umati wa wananchi wa mtaa wa Igoma B kata ya Isanga jijini Mbeya ukishuhudia uteketezwaji wa vyombo na samani za aliyekuwa Mwenyekiti wa mtaa wa Igoma A, Bwana Juma Kahawa ambaye amehamia nyumbani kwa dada yake Bi Mary James mwenye umri wa miaka 50 ambaye pia ni balozi wa mtaa huo, ndipo wananchi wa mtaa wa Igoma B kuamua kuviteketeza kwa moto kwa madai kuwa hawamtaki Bwana Kahawa kuhamia mtaani kwao kutokana na kujihusisha na imani za kishrikina.
Mtuhumiwa wa imani za kishirikiana Bwana Juma Kahawa, ambaye alikuwa Mwenyekiti wa mtaa wa Igoma A. Pichani kushoto ni siku ya mwili wa marehemu Ivon Mwakyusa ulipopatikana Novemba 21, mwaka huu, ambapo alipigiwa kura za maoni na wananchi wa mtaa wake wa Igoma A, kwa madai kuwa anajihusisha na imani za kishirikina na lawama zote kubebeshwa yeye kutokana na watoto wa mtaa huo kupotea na kufariki katika mazingira ya kutatanisha.(Picha na Kamanga na matukio, Mbeya Yetu na Chimbuko Letu)
Hitimisho:- Hata hivyo Mwenyekiti wa mtaa wa Igoma B ambako Bwana Juma Kahawa kahamia, Bwana Zacharia Vungwa amesema anasikitishwa na tabia ya balozi wa mtaa huo Bi Mary James kumpokea na kumuhifadhi mtuhumiwa wa imani za kishirikina pasipo kutoa taarifa za kuhamia kwake katika ofisi za serikali za mtaa, na hali inayotishia kuvunjika kwa amani na utulivu mtaani kwake.
No comments:
Post a Comment