Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Wednesday, June 15, 2016

Waendesha bodaboda watakiwa kufuata Kanuni,Sheria na Taratibu za Barabarani Jijini Mbeya.

Na Daudi Manongi,MAELEZO.

Mkurugenzi Mkuu Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya Bw.Godlove Mbwaji amehaidi kufanya kikao na uongozi wa waendesha bodaboda wa mkoa wa mbeya ili kuzungumzia suala la waendesha pikipiki hao kuvamia hospitali hiyo wakiwa katika kundi kubwa wakati wanapofiwa na dereva mwenzao na kusababisha usumbufu kwa wagonjwa na wakazi wa mbeya.

Mkurugenzi uyo ametoa rai kwa waendesha bodaboda hao kuwa na nidhamu wanapoingia katika hospitali hiyo kwani inatumiwa na wakazi wote wa Jiji la Mbeya na husababisha hatari kwa wagonjwa wanaohitaji huduma ya dharura hospitali hapo kwani huziba barabara yote.

Aidha ameuomba uongozi wa waendesha bodaboda hao kuchagua watu wachache wanapokuja kuchukua mwili wa mwenzao kwani itasaidia kupunguza kelele za honi na vyombo vyenyewe kwani pia kuna majirani wanaokaa katika eneo hilo wanatumia barabara hizo na hivyo kuepusha ajali.

Pia Bw.Mbwaji ametoa ushauri kwa uongozi wa waendesha bodaboda hao kuacha vitendo vya uvunjifu wa sheria na wafuate Sheria,Kanuni na taratibu za Barabarani pale mmoja wapo anapokamatwa au kugongwa kwa kutojicjhukulia sheria mkononi kumpiga aliyemgonga au kuwafanyia fujo polisi kwa kumvamia muhusika wakiwa katika makundi makubwa na hivyo kuhatarisha usalama wa Raia.

Aidha baadhi ya madereva bodaboda wa mkoa huo wamesema kuwa wamekuwa wakishinikizwa na viongozi wa matawi yao kwa madai kuwa atakayekataa kwenda kwenye maandamano atatozwa faini ya sh.50000, hata kama amebeba abiria ulazimishwa kumshusha.

No comments: