Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Monday, May 30, 2016

UJENZI WA MELI BANDARI YA ITUNGI YAGEUKA CHUO CHA UFUNDI VIJANA KUNUFAIKA ZAIDI

 
Mkandarasi mzawa,anayejenga Meli katika bandari ya Itungi Wilayani Kyela, Salehe Songolo(kushoto) akifafanua jambo kwa Waandishi wa habari kutoka Chama cha Waandishi wa habari za Utalii na Uwekezaji Tanzania (TAJATI) waliofanya ziara bandarini hapo hivi karibuni.

Mkuu wa Bandari ya Itungi Wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya, Percival Salama(katikati) akitoa maelezo kwa waandishi wa habari kutoka Chama cha Waandishi wa habari za Utalii na Uwekezaji Tanzania (TAJATI) waliotembelea bandari hiyo kuona fursa za utalii na uwekezaji.

Wanatajati wakiwa juu ya Telezo ambalo liko tayari kwa ajili ya kuanza kujengea Meli kubwa ya abiria ujenzi unaotarajiwa kukamilika Mwezi Februari mwakani.


Moja ya Meli ya Mizigo inayotarajia kukamilika mwezi Oktoba mwaka huu ikiwa katika hatua za ufungaji wa mitambo


Muonekano wa Chelezo

Wanatajati wakishuka kwenye Telezo




Mafundi wakiendelea na kazi


WanaTAJATI wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukamilisha ziara.
 
MRADI wa Ujenzi wa Meli tatu katika Bandari ya Itungi iliyopo Kyela Mkoa wa Mbeya unaofanywa na Mkandarasi mzawa kutoka kampuni ya Songolo Marine Transport Botyard umegeuka kuwa Chuo cha ufundi kwa vibarua wanaosaidia kazi.
 
Akizungumza na Waandishi wa habari kutoka Chama cha Waandishi wa habari za Utalii na Uwekezaji Tanzania (TAJATI) waliofanya ziara katika Bandari ya Itungi juzi, Mkurugenzi na mmilikiwa Kampuni ya Songolo Marine, Salehe Songolo alisema ndoto yake ni kuona anaeneza taaluma ya ufundi kwa vijana wengi.
 
Alisema kawaida vijana huajiriwa kama vibarua kwa ujira wa kuanzia shilingi Laki mbili lakini wakati huo huo huendelea kujifunza kazi za ufundi kasha hupandishwa daraja kulingana na uelewa wake na kwamba mtu ambaye hawezi kujifunza humfukuza kwa kuwa anakuwa amekosa malengo.
 
Alisema katika Miradi mitatu aliyokabidhiwa na Serikali Mwaka jana Oktoba ambayo inatarajia kukamilika Februari mwakani, vijana zaidi ya 100 wakazi wa Kyela wanatarajia kunufaika na elimu ya ufundi wanayopata kutoka kwa Mkandarasi huyo hadi kukamilika kwa miradi.
 
Aliitaja miradi inayotekelezwa bandarini hapo kuwa ni pamoja na ujenzi wa Chelezo  uliokamilika kwa asilimia 95 uliyogharimu shilingi Bilioni 2.99 kuanzia usafirishaji kutoka Mwanza hadi Kyela na uundaji wake.
 
Alisema Mradi mwingine ni utengenezaji wa Meli mbili za Mizigo zenye uzito wa tani 1000 na uwezo wa kubeba mizigo tani 566.166 kila moja ambazo zitagharimu shilingi Bilioni 11.253 na kwamba moja ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 75 na inatarajiwa kuanza kutumika mwezi Agosti Mwaka huu na nyingine iliyofika hatua ya asilimia 50 itakayokamilika mwezi Oktoba mwaka huu.
 
Songolo alisema mradi wa tatu ni ujenzi wa Meli ya Abiria na mizigo ambayo hadi sasa imefikia asilimia 30 inayotarajia kukamilika mwezi Februari mwakani inayogharimu shilingi Bilioni 10.35, na kuongeza kuwa ikikamilika itakuwa inauwezo wa kubeba abiria 200 pamoja na magari madogo 12 au makubwa na madogo matatu matatu kwa wakati mmoja.
 
Mkandarasi huyo alisema changamoto kubwa aliyokutana nayo ilikuwa ni mfumo ambao alitakiwa kujenga melihizo kuwa mpya na mgumu tofauti na mifumo aliyoitumia katika meli 48 alizozijenga nchini ambazo husimamiwa na Sumatra hivyo kuwa rahisi kuimuda kazi hiyo.
 
Alisema Meli zinazojengwa Kyela zinamfumo wa Nje na kusimamiwa na Wabelgiji hivyo alitakiwa kwenda kuchukua vibarua nchini India ambako ndiko walikozoea mfumo huo lakini kwa sababu ya uzalendo aliona ni vema kuwachukua vibarua wazawa kuwafundisha mfumo huo mpya kabla ya kuanza mradi ili taaluma ibaki nchini.
 
Alisema katika ujenzi huo jumla ya wafanyakazi 104 ambao 38 wanatoka Mkoani Mwanza na wengine wote wakitokea Kyela huku akiwa na Raia wa Kigeni wawili ambao mmoja wao ni mwalimu wa kufundisha vijana na mwingine akisaidia mawasiliano kati ya Kyela na Ubelgiji ambao ndiyo wasimamizi.
 
Baadhi ya vibarua walisema wanajivunia kupata kazi katika ujenzi wa Meli hizo kwani baada ya kukamilika kwa mradi wanauhakika wa kufungua ofisi zao katika fani mbali mbali ikiwemo uchomeleaji na uunganishaji wa vyuma pamoja na kukata.

No comments: