Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Saturday, May 21, 2016

SERIKALI YAOMBWA KUFANYIA UTAFITI ADA ELEKEZI SHULE BINAFSI

Afisa tawala na Mwanzilishi wa Shule za St. Marys Mkoa wa Mbeya, Anuciatha Ngonyani akitafakari jambo alipotembelewa na Waandishi wa Habari kutoka Chama cha Waandishi wa Habari za Utalii na Uwekezaji Tanzania (TAJATI).

Afisa tawala na Mwanzilishi wa Shule za St. Marys Mkoa wa Mbeya, Anuciatha Ngonyani akizungumza na Waandishi wa Habari kutoka Chama cha Waandishi wa Habari za Utalii na Uwekezaji Tanzania (TAJATI).

Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Utalii na Uwekezaji Tanzania (TAJATI) Ulimboka Mwakilili (mwenye suti kulia) akitoa maelezo kuhusu Tajati kwa Afisa Tawala wa Shule za St. Marys Anuciata Ngonyani,kushoto ni Katibu Mkuu wa TAJATI, Venance Matinya.

Wanafunzi wa darasa la Sita wakijifunza Kompyuta

Afisa tawala akionesha maktaba ya vitabu shuleni hapo

Afisa tawala na Mwanzilishi wa Shule za St. Marys Mkoa wa Mbeya, Anuciatha Ngonyani akiwazungusha  Waandishi wa Habari kutoka Chama cha Waandishi wa Habari za Utalii na Uwekezaji Tanzania (TAJATI) katika maeneo ya shule.

Afisa tawala na Mwanzilishi wa Shule za St. Marys Mkoa wa Mbeya, Anuciatha Ngonyani akipokea kalenda kutoka kwa Mwenyekiti wa  Chama cha Waandishi wa Habari za Utalii na Uwekezaji Tanzania (TAJATI) Ulimboka Mwakilili.

Baadhi ya Wanachama wa TAJATI wakiwa katika picha ya pamoja na Afisa tawala wa Shule za St. Marys Mbeya

Mmoja wa Wanachama wa TAJATI, Joachim Nyambo akisaini kitabu cha wageni kwenye ofisi ya Afisa tawala wa Shule za St. Marys Mbeya, anayeshuhudia ni Naibu Katibu Mkuu wa TAJATI, Patrick Kossima.

Mtunza hazina wa TAJATI, Brandy Nelson akimfuatilia kwa ukaribu mwanafunzi wa darasa la sita alipokuwa akitumia kompyuta.
 
SERIKALI inapoelekea kutoa ada elekezi kwa ajili ya shule binafsi imetakiwa kufanya utafiti kabla ili kujiridhisha kulingana na gharama za uendeshaji wa baadhi ya shule kuwa kubwa zinazoendana na huduma zake.
 
Rai hiyo ilitolewa jana na Afisa tawala na mwanzilishi wa Shule za St. Marys mkoani Mbeya, Anuciatha Ngonyani, alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari kutoka Chama cha Waandishi wa Habari za Utalii na Uwekezaji Tanzania(TAJATI) waliofanya ziara katika shule hizo zilizopo Forest jijini Mbeya.
 
Ngonyani alisema pamoja na kwamba serikali imesema haitafanya haraka katika kutoa ada elekezi kwa shule binafsi  bado inapaswa kufanya utafiti kwa kuzitembelea shule moja moja ili kujionea namna shule hizo zinavyoendeshwa na gharama zinazotumika.
 
Akitolea mfano shule zake zenye mikondo mitatu kuanzia Shule ya awali, Shule ya Msingi na Sekondari zenye mchepuo wa kiingereza, Ngonyani alisema wanafunzi wa  kutwa hupata huduma ya chakula mara mbili kwa siku pamoja na usafiri wa kwenda na kurudi majumbani kwao hivyo kutumia gharama kubwa kuendesha.
 
“Naiomba Serikali inapoendelea na mchakato ije kutembelea shule zetu ili pindi watakapotoa ada elekezi zisiumize shule zingine zikashindwa kujiendesha, binafsi sipingi kuwa na ada elekezi lakini tumetofautiana kwenye uendeshaji mimi natoa chakula na usafiri jambo ambalo shule zingine hazifanyi” alisema Ngonyani.
 
Alisema endapo kiwango cha ada kitakuwa chini sana ni dhahiri baadhi ya shule zitayumba zikiwemo St. Marys kwani watashindwa kutoa huduma nzuri kwa kununua chakula, kuwasafirisha wanafunzi, kununua vitabu na vifaa vya kufundishia pamoja na kuwalipa walimu wanaofundisha shule binafsi.
 
Aliongeza kuwa sambamba na kuwa na ada elekezi pia Serikali iangalie namna itakavyoweza kupunguza mlundikano wa kodi kwa shule binafsi jambo lililochangia kuwa na kiwango kikubwa cha ada ili kuweza kufidia kodi ambazo mmiliki wa shule anapaswa kulipia.
 
“Pia tunaviwango vikubwa na mlundikano wa kodi, hili ndo limechangia ada ziwe kubwa kwa baadhi ya shule,mfano tu hapa nalipa ada ya taka kila baada ya miezi sita shilingi laki tatu,kupima afya kila mfanyakazi elfu kumi, kodi ya majengo shlingi laki nne kwa mwaka, zimamoto laki tano kwa mwaka na kodi ya SDL kwa malipo ya wafanyakazi hivyo ukipiga hesabu ni hela nyingi tunatoa”alisema Ngonyani.
 
Aliongeza kuwa mbali na kodi hizo pia anatumia fedha nyingi kulipia Ankara za maji na umeme ambapo kila mwezi hulazimika kulipia zaidi ya shilingi Milioni tatu kwa matumizi ya maji na umeme pekee bila mahitaji mengine.
 
Aidha aliongeza kuwa hivi sasa anapata usumbufu kwa baadhi ya wazazi waliosikia kuwa kutakuwa na ada elekezi jambo linalowafanya kutolipa kwa wakati na wengine kujipangia viwango kulingana na taarifa za upotoshaji kutoka kwenye mitandao ya kijamii kwamba ada elekezi tayari imeshatolewa.
 

No comments: