Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake. |
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangiakionyesha baadhi ya tunguli zilizokamatwa na jeshi lake. |
JESHI
la Polisi Mkoa wa Mbeya limewakamata watu 15 na kuwafikisha Mahakamani
wakituhumiwa kujihusisha na upigaji wa ramli chonganishi ikiwa ni hatua ya
kuwasaka waganga wasiokuwa na vibari katika kukomesha maovu yanayotokana na
imani za kishirikina.
Hayo
yalithibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi alipokuwa
akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake ambapo alisema kesi hizo
zipo kwenye hatua mbali mbali.
Alisema
kuwa katika msako ambao ulianza tangu Machi 6, mwaka huu, Tayari Jeshi hilo
limewakamata waganga wa jadi 23 wanaojihusisha na upigaji waramli hizo
chonganishi.
Msangi
alisema watuhumiwa 15 walifikishwa mahakamani na kesi zao zipo
katika hatua tofauti na kwamba watuhumiwa sita upelelezi bado
unaendelea na mtuhumiwa mmoja taratibu zinafanywa ili aweze kufikishwa
mahakamani.
Alisema
watuhumiwa walikamatwa katika wilaya tofauti na idadi yao kwenye mabano
ambazi ni Wilaya ya Mbeya (7), Chunya(12) , momba(2),Mbozi (01) pamoja na
Kyela(01).
Aidha
Msangi alisema baadhi ya zana ambazo wamekamatwa nazo waganga hao
ni pamoja na nyara vza serikali na zana zisizokuwa na nyara zisizokuwa za
serikali .
Hata
hivyo Kamanda Msangi alitoa wito kwa wananchi kujiepusha na tabia za
kusadiki imani za ushirikina kwa kupiga ramli ili kutatua matatizo yao
kwenye jamii.
Pia
alitoa onyo kwa wananchi wanaoshirikiana kuwaficha waganga wa kienyeji
wanaojihusisha na upigaji wa ramli chonganishi ambazo zinadaiwa kuwa chanzo cha
uhalifu unaohusiana na imani za kishirikina.
Mwisho.
Picha na Mbeya yetu
No comments:
Post a Comment