Mfugaji wa Ng'ombe wa maziwa Daina Mangula (Kulia), akimwelezea Mkuu wa Mkoa wa Njombe kuhusu faida za uzalishaji ikiwa ni pamoja na soko la mbegu za malisho ya mifugo. |
Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Sarah Dumba akipata maelekezo ya mradi wa Uendelezaji sekta ya maziwa Afrika Mashariki (EADD) kutoka kwa maofisa wa mradi huo baada ya kutembelea banda la EADD. |
Mkuu
wa mkoa wa Njombe Dkt. Rehema Nchimbi amewahimiza wanawake wa Njombe kuaangalia
fursa za kujikwamua na umasikini.
Dk.
Nchimbi alitoa kauli hiyo hivi karibuni wakati wa maadhimisho ya Siku ya
Wanawake duniani ambapo kwa mkoa huo yalifanyikia katika kijiji cha Ikuna
wilayani Njombe.
Alisema
ufugaji wa ng’ombe wa Maziwa ni chachu kubwa ya maendeleo mkoani Njombe, hivyo
wafugaji wanaweza kuwa na uhakika wa kupata chakula pia inawapa
fursa nyingi za biashara kama vile kuuza ,malisho ya Mifugo, Mbegu za Malisho
na mbolea.
“Fursa
hizi zikitumiwa vizuir zitakuza uchumi wa mkoa wa Njombe na Tanzania. Maziwa ya
Njombe yanapendwa sana; imenifurahisha kujua kwamba msingi mkubwa wa ufugaji
huu wa Njombe ni wanawake” alisema Dk. Nchimbi.
Alisema
kwa Serikali na shirika la uendelezaji sekta ya Maziwa Afrika Mashariki (EADD)
watafanya kazi na wafugaji wadogo wadogo, kuinua uzalishaji wa Maziwa Njombe
ikiwemo pia kuwapa mafunzo kuhusu malisho, uhamilishaji na mafunzo ya biashara
ili waweze kuongeza kipato.
Kwa
upande wake, Ofisa mawasiliano wa mradi wa EADD nchini, Rachael Singo alisema
wanalenga zaidi kuwawezesha wanawake kwa lengo la kuonesha zaidi fursa za
kiuchumi ikiwa ni moja ya njia ya kuwaonesha wadau nafasi ya
mwanamke katika suala zima la kukuza uchumi kwa kaya na jamii kwa ujumla.
Alisema
EADD itaendelea kushirikiana na Serikali katika juhudi za kuondoa
umaskini, kuondoa baa la njaa, uhakika wa kupata chakula cha kutosha na ustawi
endelevu wa wananchi na kujiongezea kipato kwa njia ya kushiriki kazi za
uzalishaji wa maziwa.
Singo
alisema mradi huo ambao utatekelezwa ndani ya miaka mitano, unalenga Kufikia
kaya 35,000 za wafugaji wa ng’ombe wa maziwa katika Nyanda za Juu Kusini
kwenye mikoa ya Iringa, Njombe na Mbeya, ambapo asilimia 30 ya wafugaji hao ni
wanawake .Kupitia Mnyororo wa thamani wa uzalishaji wa Maziwa ; wafugaji
watapata fursa nyingi za biashara kwenye vitovu vya Maziwa chini ya mradi wa
EADD”
Naye
Afisa wa Maendeleo ya Jamii na Jinsia wa Mradi wa EADD, Lightness Munisi
alisema mwanamke ni mdau mkubwa wa maendeleo katika jamii, hasa kwenye
shughuli za ufugaji , hivyo siku ya wanawake duniani wanaitumia kuwahamasisha
wanawake kutambua fursa za kiuchumi zitokanazo na ufugaji wa kisasa wa
ng’ombe wa maziwa ili kuondokana na dhana ya utegemezi.
Mradi
wa Uendelezaji Sekta ya Maziwa Afrika Mashariki(EADD) ; ni mradi
unaotekelezwa na shirika la Mitamba Duniani ( Heifer International ) kwa
kushirikiana na shirika la International Livestock Research Institute
(ILRI), TechnoServe, ABS na World Agroforestry Centre. Mradi huu unawapa
wafugaji fursa ya kujikwamua kimaisha kupitia mnyororo wa thamani wa maziwa
Mwisho.
No comments:
Post a Comment