Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Deodatus Kinawiro, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Chunya na Mwenyekiti wa kikao cha maandalizi ya Nanenane akisisitiza jambo kwa wajumbe waliohudhuria kikao hicho.
Mmoja wa Wajumbe wa Sekretarieti ya Nanenane Kanda, Hamza Mvano, akiwasilisha mada katika kikao cha maandalizi ya nanenane.
Wajumbe wa kikao cha maandalizi ya nanenane 2014 wakifuatilia kwa makini yaliyoandikwa kwenye makabrasha wakati wa kikao kilichofanyika katika ukumbi wa JKT Nanenane.
***********
MAANDALIZI
ya Sherehe za sikukuu za wakulima nanenane Kanda ya Nyanda za juu Kusini bado
yanasuasua licha siku kubakia chache kutokana na kukosekana kwa fedha.
Hayo
yalibainishwa jana na Mjumbe wa Sekretarieti ya Nanenane Kanda, Hamza Mvano,
wakati wa kikao cha mwisho cha maandalizi ya sherehe hizo kilichofanyika katika
ukumbi wa JKT uliopo ndani ya Viwanja vya John Mwakangale Uyole jijini Mbeya.
Mvano
alisema hadi kufikia Julai 24, mwaka huu idadi ya wadau waliothibitisha
kushiriki maonesho ya mwaka huu imefikia 363 kati ya 399 waliopewa mwaliko.
Alisema
mbali na washiriki kutokamilika lakini bado michango kwa ajili ya kufanikisha
maonesho na sherehe za Kanda kwa mwaka huu imefikia kiasi cha shilingi Milioni
16.5 wakati malengo ni kukusanya Shilingi Milioni 181.
Alisema
makusanyo hayo ni sawa na asilimia 9 hivyo kutia shaka kufanyika kwa ufanisi
katika maonesho hayo licha ya wadau ambao ni Halmashauri na Ofisi za Makatibu
tawala wa Mikoa kupewa taarifa mapema za uchangiaji.
Alivitaja
viwango ambavyo vinavyotakiwa kuchangwa na Halmashauri kuwa ni Shilingi Milioni
mbili kila moja na Ofisi za Makatibu Tawala wa Mikoa shilingi Laki tano.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Kikao hicho, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Deodatus
Kinawiro, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Chunya, alisisitiza Halmashauri zote
kuhakikisha zinamalizia michango yao mapema kama wanavyopaswa.
Alisema ni aibu kwa mikoa ya Kanda ya
Nyanda za juu kusini kushindwa kufanya maonesho kutokana na ukosefu wa fedha
wakati Mikoa hiyo husifika kitaifa kwa uzalishaji mkubwa na kuongoza katika
kuchangia pato la Taifa.
Maonesha
hayo ambayo hufanyika kila mwaka katika viwanja vya John Mwakangale Uyole
jijini Mbeya huandaliwa na Chama cha Wakulima Tanzania (TASO).
Akizungumzia
maandalizi ya mwaka huu, Katibu wa TASO kanda ya Nyanda za juu kusini,
Ramadhani Kiboko, alikiri kusuasua kwa maandalizi ya sikukuu za wakulima
nanenane mwaka huu tofauti na miaka iliyopita.
Kiboko
alisema kawaida kila mwaka maandalizi na shamla shamla za washiriki kuanza
kuandaa maeneo yao pamoja na vipando huanza Juni 30 lakini hadi sasa hakuna
kinachofanyika pamoja na jitihada za kuanza kutumika kwa stendi mpya.
Alisema
tangu mwezi Machi mwaka huu TASO ilitoa barua za mialiko ya kushiriki maonesho
ya mwaka huu kwa washiriki 399 ambao ni pamoja na Halmashauri za Kanda, Taasisi
za Serikali, bodi za mazao, Taasisi za majeshi,Wizara za Serikali na vituo vya
utafiti.
Pia
alitoa wito kwa wafanyabiashara mbali mbali kutumia Uwanja wa John Mwakangale
katika biashara zao kwa kuendeshea magulio au minada ya bidhaa mbali mbali
kipindi ambacho kunakuwa hakuna maonesho.
Na Mbeya Yetu
No comments:
Post a Comment