Hatimaye Madrasa Bora ya Ijti-had
Islamiya ya Isanga Mbeya ambayo imefanya vizuri kwa kuwawezesha wanafunzi
kuhifadhi na kusoma Koran Tukufu wamezawadiwa Pikipiki aina ya Boxer namba T
540 CYM kwa ajili ya mradi wa kiuchumi wa Madrasa hiyo.
Akitoa msaada wa Pikipiki hiyo Muumini
wa Kiislamu mkoani Mbeya Shekhe Adam Safari alisema mbali na kumpa moyo Ustadhi
wa madrasa hiyo Pikipiki hiyo itakuwa ni sehemu ya mradi wa Madrasa hiyo kwa
ajili ya kujiongezea kipato.
‘’Hii itakuwa ni mradi wa Madrasa
kujiongzea kipato, itafanya kazi na fedha zake zitaingia kwenye mfuko wa
Madrasa hiyo, tunaamini itatumika kwa ajili ya kuendeleza dini,’’alisema Shekhe
Safari.
Aliongeza kuwa mara nyingi waislamu
wanapopata mradi wa kuingiza fedha inakuwa ndio chanzo cha migogoro na kuwa
anaamini pikipiki hiyo haitakuwa chanzo cha migogoro bali itakuwa ni chanzo cha
mafanikio na maendeleo ya Uislamu.
Akizungumzia mradi huo, Ustadh wa Madrasa
hiyo, Mussa Seif alisema kuwa utasaidia katika maeneo mengi kutokana na
changamoto zilizopo katika Madarsa hiyo kama vile ujenzi na Posho ya Ustadhi na
kuwa anaamini mradi huo ukisimamiwa vyema utachangia maendeleo ya Madrasa hiyo.
Alisema kuwa siri ya mafanikio ya
madrasa yake imetokana na ushirikiano uliopo baina ya wazazi ambapo pia watoto
wamekuwa wakiandaliwa kisaikolojia na kuhamasika kwa kujituma kutokana na
ufuatiliaji wa karibu wa masomo yao.
Kwa hisani ya Rashid Mkwinda Blog
|
No comments:
Post a Comment