MASHABIKI wa Timu ya Mbeya City tawi la
Sido jijini Mbeya wameipongeza timu hiyo kwa mafanikio waliyoyapata katika
Msimu uliopita wa Ligi kuu Bara uliomalizika kwa timu hiyo kuibuka mshindi wa
tatu.
Pongezi hizo zilitolewa jana katika
Sherehe iliyoandaliwa na Tawi hilo zilizofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Gr
iliyopo Soweto jijini Mbeya na kudhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania(TBL)
iliyohudhuriwa na wachezaji wote wa Mbeya city pamoja na viongozi na mashabiki.
Wakizungumza katika sherehe hizo.
Mashabiki hao walisema timu hiyo imeweza kuzitikisa timu kongwe na kubwa hapa
nchini hivyo hawana budi kutoa ushirikiano kwa timu yao katika msimu ujao ili
iweze kuibuka katika nafasi mbili za juu.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Timu ya
Mbeya City, Musa Mapunda, akizungumza kwa niaba ya Meya wa Jiji la Mbeya,
Atanus Kapunga, alilipongeza Tawi la Sido kwa kuonesha uzalendo kwa timu yao na
kuwa chachu ya mafanikio ya timu.
Alisema mashabiki wa Mbeya city tawi la
Sido limekuwa likishiriki shughuli nyingi za timu ikiwa ni pamoja na kusafiri
na timu kila timu inapoenda kwa gharama zao wenyewe tofauti na matawi mengine
ambayo hutaka kuchangiwa.
Alisema mafanikio ya Mbeya city
hayapendwi na watu wengi hususani wapinzani wao hivyo ni vema mashabiki
wakaunga mkono kwa nguvu zote ili kuhakikisha timu inafanya vizuri tofauti na
wao wanavyotaka.
Aidha katika Sherehe hizo Wachezaji wa
Mbeya city walitambulishwa mbele ya mashabiki pamoja na kukabidhiwa zawadi
zilizotolewa na Abubakar Masoli,ambaye ni Meneja matukio wa Kampuni ya Bia
(TBL) Mbeya.
Naye katibu wa Mbeya City, Emmanuel
Kimbe, alisema shughuli zote za kiuchumi za timu hiyo zitashirikisha moja kwa
moja mashabiki na matawi pamoja na Halmashauri ili kuhakikisha ushirikiano
unadumu kwa mafanikio ya timu.
Mwisho.
Na Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment