Afisa wa Jamii Mji Mdogo wa Makongolosi, Nkongoki Ezekiel kwa niaba ya Mbeya yetu blog akimkabidhi mtoto Elizabeth Tanzania mafuta chupa moja ya kujikinga na jua
WATOTO
wenye ulemavu wa ngozi(ALBINO) wilayani Chunya Mkoa wa Mbeya wanaomba msaada wa
kupatiwa mafuta ya kuzuia mwanga wa jua unaoathiri ngozi zao.
Maombi
hayo yalitolewa na zaidi ya watoto sita wenye ulemavu wa ngozi wanaoishi
Makongolosi Wilaya ya Chunya mkoani hapa ambao wanakabiliwa na ukosefu wa
mafuta ya ngozi,miwani ya kusomea na kofia ili kuweza kukabiliana miale ya jua.
Mama
Mzazi wa watoto hao, Sophia Edward(30) alisema wanawe Lusekelo Tanzania(13)
anayesoma darasa la saba na Elizabeth Tanzania(8)anayesoma darasa la tatu
wanakabiliwa na ukosefu mafuta,kofia na miwani ya macho kwa muda mrefu hivyo
kuwafanya watoto hao kuwa na wakati mgumu kutokana na joto kali hali iliyopelekea
ngozi zao kuharibika.
Kwa
upande wake Afisa wa Jamii Mji Mdogo wa Makongolosi, Nkongoki Ezekiel
alisema kuwa watoto hao kwa mara ya mwisho walipata mafuta miezi sita
iliyopita.
Alisema
mafuta hayo ni adimu na wao hawana namna yoyote ya kufanya hivyo kuwaomba
wasamaria wema wenye mafuata,miwani na kofia kuwasaidia ili wakabiliane na
changamoto zinazowakabili.
Aidha
alisema mbali ya changamoto hiyo watoto hao wamekuwa na maendeleo duni katika
masomo kutokana na udhaifu wa kuona vema hivyo kushindwa kuona vizuri na
wingi wa wanafunzi katika darasa kunawafanya kuwa nafasi chini.
Mama
mzazi wa watoto hao alisema kipato duni kimesababisha watoto kuwa na matokeo
hafifu kwani kipato chao kinatokana na Baba mzazi Bwana Tanzania
Mwakatobe(46)kutegemea uchimbaji wa madini ndipo wapate riziki hivyo kushindwa
kuwapeleka shule maalumu.
Mwisho.
Na Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment