Mahakama
Kuu Kanda ya Mbeya, imebatilisha hukumu ya kifungo cha miaka 30 jela na
viboko 12 aliyokuwa akiitumikia Mchungaji wa Kanisa la EAGT la Iwambi Jijini
Mbeya, Daniel Mwasumbi(57) aliyekuwa akikabiliwa na kesi ya ubakaji na
kumpa mimba mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Itende Neema Beni(19) jijini hapa.
Mchungaji
Mwasumbi alihukumiwa kifungo hicho, Januari 2 mwaka huu na mahakama ya Wilaya
ya Mbeya na Hakimu Gilbert Ndeuruo na Serikali kuwakilishwa na wakili Achiles
Mulisa, ambapo Mahakama ilimtia hatiani Mchungaji katika makosa kinyume cha
sheria kifungu cha 130(2)e na 131(1) sura ya 16 ya sheria iliyofanyiwa
marekebisho mwaka 2002.
Awali
Mchungaji Mwasumbi alikuwa akitetewa na Wakili wa kujitegemea Victor Mkumbe
ambapo ilidaiwa kutenda makosa hayo kati ya Januari 2008 hadi 2011 ambapo
alimpa ujauzito na kumzalisha mwanafunzi huyo watoto wawili wa kiume kwa
nyakati tofauti hivyo kumkatisha masomo kinyume cha sheria.
Katika
Rufaa hiyo Mchungaji Mwasumbi alikuwa akitetewa na Wakili wakujitegemea
Benjamin Mwakagamba kutoka Dar es Salaam wakati Serikali iliwakilishwa na
Wakili Prosister Paul.
Akisoma
hukumu ya rufaa hiyo, Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya, Atuganile Ngwala,
alisema kuwa sababu zilizowasilishwa kwenye mahakama hiyo na Wakili
wa upande wa utetezi zilidhihirisha kuwa kulikuwa na ukiukwaji wa kisheria
kwenye hukumu hiyo.
Jaji
Ngwala ambaye alitumia takribani saa 1:15 kusoma huku hiyo alisema katika
utoaji wa hukumu hiyo haukuzingatia vipengele muhimu vya kisheria
viilivyotumika na mahakama ya wilaya kumtia hatiani Mchungaji Mwasumbi.
“katika
rufaa hii ni kweli kuna mambo mengi ambayo yanaonekana kukiukwa katika utoaji
wa hukumu, kama zilizovyoweza kuanishwa na wakili wa utetezi hivyo na mimi
nakubaliana na wakili Mwakagamba (wakili wa utetezi) kwamba kulikuwa na
ukiukwaji wa kisheria kwenye hukumu hiyo” alisema
Aliongeza
kwamba kama ilivyoelezwa na wakili Mwakagamba, muda wa lilitopotekea
tukio hilo na liliporitiwa kwenye vyombo vya usalama unaonekana kuchelewa na
kukinzana, lakini pia ushahidi ulitolewa mahakamani hapo na Mhanga
ulionekana kujichanganya hivyo haujaonesha mrufani kutenda kosa hilo’.
Awali
Jaji Ngwala alimwita mchungaji Mwasumbi kuwa ni mende, na ni mtu hatari sana
katika jamii kwa kosa kama hilo na hafai kuwa katika jamii jambo lililowafanya
watu waliokuwa wakifuatilia mwenendo wa hukumu hiyo kuanza kuinamisha vichwa chini
akiwemo Katibu wa Kanisa la Uinjisti Bwana Mwakasole.
Lakini
baadaye, Jaji Ngwala alionesha hisia zake kwamba kutokana na
kujichanganya kwa ushihidi hususani wa shahidi namba moja ambaye ni binti
aliyefanyiwa kitendo hicho hivyo kumtoa hivyo na haonekani kama ana kosa.
Alisema
‘Nasema hivi mtu huyu alikuwa ni mende na ni hatari sana katika jamii asiyefaa
kwa namna yoyote ile na anastahili adhabu kali laiti kama ingethibitika hivyo,
lakini hapa ushahidi umeshindwa kuthibitisha hili hivyo ana haki ya kuachiwa
huru’.
Hata
hivyo, Jaji Ngwala alisema kuwa kwa upande wa Jamhuri ambao ulikuwa ukiongozwa
na wakili wa Serikali, Prosister Paul una haki zote za kukata rufaa na kesi
kuanza upya endapo utaona haujaridhika na hukumu hiyo.
Wakili
aliyekuwa akimtetea Mchungaji Mwasumbi alisema kuwa katika rufaa ya mteja wake
aliwasilisha sababu saba za kupinga hukumu hiyo ambapo alidai kuwa hakimu
wakati wa kutoa hukumu hiyo alikosea kisheria na haki muda wa kuripotiwa kwa
shauri hilo kwa vyombo vya usalama na lilipotokea ulikinzana na kwamba
aliegemea kwa ushahidi wa Mhanga tu.
Sababu
zingine alidai kuwa hakimu aliegemea katika ushahidi au vidhibiti ambavyo
awali alivikata mwenyewe, pia alidai kuwa hakimu hakuangalia uhalisia kosa
lenyewe na badala yake alionekana kutoa maoni yake binafsi.
Lakini
sababu nyingine wakili Mwakagamba alisema kuwa hakimu huyo, aliegemea ushahidi
ambao ulijichanganya, wendesha mashtaka walishindwa kuwapeleka mahakamani
hapo mashahidi wa msingi katika kesi hiyo, hakimu aliegemea upande wa
vyeti vya watoto wawil waliodaiwa ni wa Mchungaji Mwasumbi ambapo vyeti
vilidurufiwa (photocopy) na si vyeti halisi na mwisho hakimu huyo alitoa
hukumu ambayo haikufuata mtiririko uliosahihi wa mashahidi husika.
Akizungumza
na Mbeyayetu blog, mtoto wa Mchungaji Mwasumbi, Elizabeth Mwasumbi
alisema anamshukuru Mola kwa kumwezesha Jaji Ngwala kwa kutenda haki katika
rufaa ya baba yake.
Alisema;
’Mimi na wenzangu tulikuwa na wakati mgumu sana pindi baba yetu akiwa ndani,
kwani mimi niliathirika sana kiafya na kiuchumi nilishindwa kufanya shughuli
yoyote kutokana na mawazo lakini namshukumuru Mola kwa kutenda haki’.
Hata
hivyo nje ya Mahakama ndugu na jamaa waliofurika kusikiliza hatma ya Rufaa hiyo
waliokuwa na hamu ya kumlaki kwa furaha Mchungaji Mwasimbi ambaye pia ni
mwimbaji wa nyimbo za Injili kushindwa kutokana na Maafisa wa Magereza
kumpeleka Gerza la Ruanda kukamilisha taratibu za Magereza
Na Ezekiel Kamanga
Mbeya yetu
|
1 comment:
I real thank God, fir answering our prayers,be been praying over this matter & personally am so happy to hear this good news about Lev Mwasumbi.Thank you Jesus.
Post a Comment