Wazazi wa mtoto Adorotea miezi mitatu iliyopita wakiwa uwanja wa ndege mbeya wakisubiria ndege kuelekea DSM kwa upasuaji wa mtoto huyo.
Mtoto
Adorotea Emmanuel Njavike mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu aliyekuwa
anakabiliwa na majeraha ya moto na kusababisha ulemavu wa shingo amafanyiwa
upasuaji katika Hospitali ya CCBRT iliyoko Dar es Salaam na sasa hali yake
inaendelea vema.
Mama
mzazi wa mtoto huyo Milika Kaberege(35) alisema kuwa mwanawe alipata majeraha
hayo baada kuangukia motoni mwezi Octoba mwaka jana wilayani Njombe na kupatiwa
matibabu Mbeya bila mafanikio.
Baada
ya kuendelea kukosa matibabu yakinifu ndipoalionwa na vyombo mbalimbali vya
habari na habari zake kuandikwa ndipo Bohari ya Madawa nchini MSD
walipojitokeza kutoa usafiri wa ndege kutoka Mbeya kwa kushirikiana na Kikundi
cha Wanawake ambaio walimfikisha CCBRT mwezi Machi mwaka huu.
Milika
alisema kutokana na juhudi kubwa za Madaktari wa Hospitali hiyo mwanawe
amefanyiwa upasuaji mara mbili na kwamba hali yake inaendelea vema na bado
juhudi za Madaktari hao zinaendelea kurekebisha viungo vya mwanawe ikiwa ni
pamoja na mikono yote miwili ilyopata majeraha.
Mama
huyo ameshukuru Asasi mbalimbali zilizohangaikia matibabu ya mtoto wake
wakiwemo waandishi wa habari wa Mbeya yetu ambao wamefuatilia maendeleo ya mtoto hata kufika
Wodini kumjulia hali hivi karibuni na ameendelea kupata Faraja siku hadi siku
kutoka kwa wadau wanaofika Hospitali.
Aidha
amesema huenda mwanawe akatoka hivi karibuni baada ya kufanyiwa upasuaji wa
mwisho wa mikono na haamini kwamba mwannae ambaya alikuwa akipata shida hata
kula chakula na sasa anaweza kula na kutokana na juhudi kubwa za madaktari
mtoto wake hivi sasa ameanza kutembea.
Mama
Milika ametoa wito kwa wazazi na walezi wenye watoto wenye ulemavu kuacha
kuwaficha ndani bali wawapeleke Hospitali kama ya CCBRT ambao wanafanya kazi
ngumu ya kurekebisha viungo na wagonjwa kurejea katika hali ya kawaida kutoa
wito kwa wagonjwa kutokata tamaaa hali.
Upasuaji
wa awali wa Adorotea ulifanyika Machi 21 mwaka huu wakati ule wa pili
ulifanyika Mei 16 mwaka huu na upasuaji wa tatu utafanyika wakati wowote
kuanzia sasa na kuruhusiwa kurudi nyumbani.
Kwa
yeyote anayeguswa kutoa msaada wa hali na mali anaweza kumpatia kupitia simu
yake ya mkononi namba 0753913472.
Na Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment