Waumini
wa Makanisa ya PCGT(Pentecoste Church of God Tanzania)linaloongozwa na Askofu
Anyimike Mwakalasya na PEWOMI(Pentecostar World Wide Ministries)linaloongozwa
na Askofu Fredrick Silumbwe wamemaliza mgogoro uliokuwa Mahakamani na kudumu
miaka mitatu bila muafaka.
Mgogoro
huo umetatuliwa na Asasi isiyokuwa ya kiraia ya Muungano wa Jamii
Tanzania(MUJATA)na kuridhia kufuta kesi iliyokuwa Mahakamani bila masharti
yoyote ikihusisha pande hizo mbili baada ya waumini hao kutishiana kuuana na
kujengeana chuki kwa muda mrefu.
Mapatano
hayo yamefanyika mbele Viongozi wa MUJATA akiwemo Mwenyekiti Soja
Masoko,Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili Chifu Shadrack Merere na wajumbe wanne
wa wanawake ambapo pande hizo mbili ziwekeana saini mkataba wa kumaliza
mgogoro.
Ugomvi wa waumini hao ulitokana
na kuvuliwa madaraka kwa Askofu Fredrick Silumbwe hivyo yeye kuamua kuanzisha
Kanisa jipya la PEWOMI hali iliyowafanya baadhi ya waumini kuwekwa mahabusu
hali iliyozidisha machafuko na kuchochea chuki miongoni mwa waumini.
Na Mbeya yetu
|
2 comments:
Hii ingekua hatari sana,bora wamepatana pasipo kumwaga damu ya mtu yeyote!!!kama ingemwagika damu,mapatano yasingefanyika maana kungekuwa na visasi vikubwa aana!!!
MUNGU NA UCHIFU WAPI NA WAPI WANA MBEYA?????
Post a Comment