Afisa ustawi wa jamii Wilaya ya Mbeya, Magdalena Songoma akitoa mada kwenye Semina ya Watumishi na makundi maalum ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya.
Washiriki wa Semina wakifuatilia kwa makini mada zinazotolewa.
Washiriki wa semina wakijadiliana kwenye makundi.
.Mratibu wa Ukimwi Wilaya ya Mbeya, Kelvin Kisoma akifuatilia jambo.
Mwenyekiti wa Darasa hilo, Felix Lyaniva akisisitiza jambo kwa washiriki wa Semina.
Wawakilishi wa makundi wakiwasilisha kazi kwa washiriki wa semina hiyo.
Katibu wa dawati la Jinsia kutoka Jeshi la Polisi, Pudensiana Baitu akichangia mada kwenye Semina hiyo.
HALMASHAURI ya Wilaya ya Mbeya
kupitia kitengo cha Ukimwi na Ustawi wa Jamii imeendesha mafunzo ya Siku mbili
kwa Watumishi wa Halmashauri hiyo pamoja na makundi mengine kuhusu Unyanyasaji
wa kijinsia na ukatili dhidi ya Watoto vinavyochangia kuwepo kwa maambukizi
mapya ya Ukimwi.
Mafunzo hayo yaliyoanza Mei 29
na kukamilika Mei 30, Mwaka huu yalifanyika kwenye ukumbi wa Kituo cha Walimu
kilichopo Mbalizi katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya.
Mratibu Kitengo cha Ukimwi
Wilaya ya Mbeya, Kelvin Kisoma, amesema lengo la mafunzo ni kutoa elimu kwa
watumishi kuanzia ngazi ya kata hadi Halmashauri ili nao wakawaelimishe watu
wao juu ya ukatili wa kijinsia unavyochangia maambukizi mapya ya Ukimwi.
Aliwataja walengwa wa Semina
hiyo kuwa ni pamoja na Viongozi wa Dini kutoka kila kata, Watu mashuhuri,
viongozi wa Siasa, madiwani, maafisa maendeleo ya Jamii, Asasi
zinazojishughulisha na jinsia na Ukimwi, Maafisa Tarafa, Walemavu na wakuu wa
Idara za Halmashauri.
Aidha alisema viongozi hao
wanatoka katika Kata za Utengule Usongwe, Mshewe, Tembela, Igoma, Inyala,
Ilembo,Iwiji, Itewe, Bonde la Songwe,Swaya, Iyunga mapinduzi,Ihango,Ijombe,
Santilya, Itawa na Nsalala.
Aliongeza kuwa moja ya vigezo
au visababishi vya maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi ni pamoja na Ubakaji,
Unyanyasaji na Mafarakano katika ndoa.
Kwa upande wake Afisa Ustawi wa
Jamii Wilaya ya Mbeya,Magdalena Songoma, alisema ni vema jamii ikasaidia kutoa
elimu kwa wengine kuhusu kuzuia vitendo vya ukatili na sio kusubiri hadi
vitendeke ndipo watoe taarifa.
Aliongeza kuwa lengo la mafunzo
hayo ni kuifanya jamii ielewe juu ya visababishi vya ukatili, ukubwa wa tatizo
na jinsi ya kukabiliana nalo ikiwa ni pamoja na kujua hatua za kufuata hali
hiyo inapotokea.
Naye Katibu wa dawati la Jinsia
kutoka Jeshi la Polisi, Pudensiana Baitu, alisema ndani ya kipindi cha miezi
mitatu imeonekana wanaume ni wengi wanaofanya vitendo vya ukatili dhidi ya
watoto wa kike.
Alisema asilimia kubwa watoto
wa kike hufanyiwa vitendo vya ukatili ambavyo ni ubakaji unaowakumba watoto
wenye umri kati ya miaka 15 hadi 18 kutokana na mabadiliko ya kimwili.
Na Mbeya Yetu Blog.
No comments:
Post a Comment