Kampuni ya ndege ya fastjet imetangaza kuwa itaongeza safari zake za anga kati ya Dar na Mbeya kutoka mara tatu kwa wiki hadi kufikia mara saba kwa wiki ifikapo katikati ya mwezi wa disemba.
Kwa mujibu wa taarifa kupitia mtandao wa kampuni hiyo safari za anga kati ya Mbeya na Dar zimekuwa ni maarufu kutokana na idadi kubwa ya abiria na hivyo basi kampuni hiyo imeamua kuongeza safari zake. Kuanzia tarehe 24 Novemba kutakuwa na safari za jumapili na ifikapo tarehe 17 Disemba itaongeza safari nyingine tatu na hivyo kufanya jumla ya safari saba kwa wiki ikimaanisha kila siku ya wiki kutakuwa na safari ya shirika hilo kati ya Dar na Mbeya.

1 comment:
Kwanini hamtaji bei halisi, sijui lolote kuhusu kodi za serikali kwa safari za ndege. Naomba bei kamili ninayotakiwa kuulipa kwa safari huu mwingine ubabaishaji
Post a Comment