Alisema Jeshi la Polisi kupata taarifa za
Kinterejensia waliweka mitego mbali mbali na kufanikiwa kuwanasa watu hao
wakiwa kwenye gari lenye namba za usajili T 911 BUG aina ya Toyota
Spacio ambapo baada ya kusimamishwa katika eneo hilo wakitokea Kyela kuelekea
Jijini Mbeya.
Alisema baada ya kusimamishwa ghafla walianza
kurusha risasi ovyo ambapo Askari walijibu mapigo na kufanikiwa
kuwajeruhi wote watano ambapo waliwafikisha katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya
kwa ajili ya Matibabu lakini Daktari alithibitisha kuwa tayari walikuwa
wamekufa.
Aliongeza kuwa baada ya kufanyiwa upekuzi
walikutwa na Silaha mbili ambazo ni bunduki aina ya SMG 848628 ambapo kwenye
magazine zilibaki risasi 16 na bunduki nyingine aina ya Mark III yenye namba
94695J ikiwa na risasi mbili pamoja na Koa za Shaba.
Kamanda Diwani ameongeza kuwa taarifa za
Kinterejensia zilieleza kuwa majambazi hayo yalijipanga kufanya uhalifu katika
maeneo ya Ushirika, Tukuyu Mjini Wilayani Rungwe pamoja na Eneo la Uyole Jijini
Mbeya.
Aidha alisema majina yao wala makazi yao
hayakuweza kujulikana maramoja ambapo miiliehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa
ya Mbeya na kutoa wito kwa wananchi kufika Hospitalini hapo kwa ajili ya
kuwatambua ndugu zao ili wakabidhiwe kwa taratibu za mazishi.
Pia anatoa wito kwa wananchi wenye taarifa
zinazohusu uhalifu kuzitoa katika mamlaka zinazohusika kwa wakati ili zifanyiwe
kazi.
Picha na Mbeya yetu
5 comments:
Hongereni jeshi la polisi kwa kazi mnayofanya,lakini bado napata mashaka taarifa zinasema walikuwa wakirushiana risasi na polisi na ndipo wakajeruhiwa ambapo baadaye daktari alithibitisha kuwa wamefariki.Nikiangalia gari sioni alama yoyote ya majibizano ya risasi!au walishuka chini ndo wakaanza kujibizana na polisi?
Mdau wa mbeya yetu kutoka Mwanza.
ok Nalipongeza jeshi la Police Tanzania na hususani Mbeya, ila Mipango makini iwepo kuwafuatilia wahalifu wengine waliojificha,na si kusubiri mpaka mpate taarifa mahali.Pia naliomba Jeshi letu la Police liwe na ukaribu na wananchi hata kwa matatizo ya kisiasa au kijamii, Naamini nchi itakuwa na utulivu na amani, wako Ayubu J.M kutoka Dar es salaam
Katika akiri ya kawaida nashindwa kuelewa au kuamini moja kwa moja taarifa ya jeshi la polisi hasa pale inpodaiwa kuwa kulikuwa na urushianaji lisasi, hamna hata kiashilia kimoja kinachoonyesha urushianaji risasi kwa kuangalia gari yenyewe iliyokuwa ikitumiwa na wanaosemekana kuwa majambazi lakini pia majeruhi ya hao wanaosemekana kuwa majeruhi naona ni kama yanahusisha kupigwa si tu kwa risasi, sijui liko vipi hili lakini hebu tuwe tunapewa taarifa ambazo ni sahihi na jeshi la polisi hii itaongeza imani kwa wanainchi lakini pia itaongeza ushirikiano,
tuambieni ukweli kuhusu hawa watu.
ha ha wanaotaka kujua zaidi hoja yao ni kutoamini kuwa haya ndiyo yaliyofanywa na hawa nami namashaka na wote walioeleza kuwa hawana imani inawezekana ni wenzao ha hawa majambazi polisi fuatilia vizuri hawa inawezekana ni wale wale, polisi sio vichaa kuwa wanachukua maamuzi yasio sahihi, tambueni kuwa mungu amechoka ameamua kuhukumu hapa hapa duniani acheni ushabiki usio na maana ungekuwa umefanyiwa wewe haya yote ungesema pongezi kwa polisi mkoa wa mbeya mnastahili, kikwete awatazame kwa kazi nzuri ,
Majambazi ni kweli yauwawe maana nilishudia tukio moja la uporaji eneo la sinza kwenye wakala wa mitandao ya pesa wakimuua mama mmja oliyekuwa akifanya shuhuli za pesa kwenye kibanda cha tigo,airtel,na voda.walimuuwa na kupora milioni kumi,kwa hiyo nakipongeza kitendo cha jeshi la polisi kutumia nguvu kuwatokomeza wahalifu hawa.
Post a Comment