Picha ya pamoja
BAADHI ya Wananchi Mkoani Mbeya wamelipongeza
Jeshi la Polisi Mkoani hapa kwa kuendelea kusambaratisha na kumaliza kabisa
mtandao wa ujambazi kutokana na majambazi wengi kukamatwa na wengine
kuawa.
Pongezi hizo zimekuja Siku moja baada ya Jeshi
hilo kuwauwa watu watano wanaosadikiwa kuwa ni majambazi katika majibizano ya
kurushiana risasi kati ya Askari na majambazi hayo katika tukio lililotokea
katika kijiji cha Garijembe Wilaya ya Mbeya.
Katika kuhakikisha Jeshi hilo linaendelea
kufanya kazi katika mazingira mazuri na kwa mafanikio na kuunga mkono
juhudi zao, Wadau mbali mbali leo wamejitokeza kulichangia jeshi
hilo katika Hafla iliyofanyika katika viwanja vya ofisi ya Kamanda wa Polisi
Mkoani hapa.
Hafla hiyo ambayo mgeni rasmi alikuwa ni
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Mkuu
wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro Jumla ya Shilingi Milioni 28 zilipatikana
vikiwemo vifaa mbali mbali.
Mwenyekiti wa kikosi cha Mafanikio cha
kuchangisha fedha na michango ya kuliwezesha Jeshi la Polisi kufanya kazi
katika Mazingira mazuri, Julius Kaijage amesema Askari wa Jeshi la Polisi
wanafanya kazi katika mazingira magumu hivyo ni jukumu la kila mwananchi
kuhakikisha analiwezesha kwa hali na mali.
Katika Hafla hiyo Jumla ya Pikipiki tano
zilinunuliwa ambapo kati ya hizo Tatu zimetolewa na Benki ya Nmb kwa thamani ya
Shilingi Milion 5.4, wakati kamati ikinunua pikipiki Mbili kwa Thamani ya
Shilingi Milioni Moja na Laki Nane.
Mbali na michango hiyo pia Wakala wa Majengo mkoa
wa Mbeya (TBA) imetoa mabati 22 ya Geji 28 yenye thamani ya Shilingi 460,000/=,
pia kamati ya Mafanikio imenunua Matairi nane yenye thamani ya Shilingi Milioni
3,020,000/=,pamoja na mafuta kwa ajili ya magari ambayo ni Lita 360 kwa Mwaka
zilizoahidiwa na kampuni ya G4S.
Mbali na pongezi hizo Wananchi hao wamemshauri
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani mbali na kupambana na uhalifu
katika Mkoa wa Mbeya na kuwasisitiza watu wanaofanya shughuli zisizokuwa na
uhalali kuacha mara moja au kuhama Mkoa pia wapendekeza kufanya ziara za
kushtukiza katika Vituo vidogo vya Polisi.
Kwa upande wake Kamanada wa Polisi Mkoani hapa Diwani Athumani amewapongeza wadau mbalimbali waliojitokeza kulisaidia jeshi
hilo ambapo amewahahakikishia wananchi wa mkoa huu kuwa kwa sasa mkoa wa mbeya
upo katika mazingira salama kutokana na ushirikiano uliopo kati ya wananchi na
jeshi hilo .
Na Mbeya yetu
|
2 comments:
Asante kwa habari.Ila nimeshtuka huyo mama na hiyo make up yake huo wanja sijui ndio wanaita Sina Mume au Utajiju !!!!. Jifunzeni wanawake kujipamba wala hamvutii kwa style hii.
SO funny! Yea bora usitie makeup kama hujuwi kujipamba red/ pink eyebrows! That's a no no
Post a Comment