Wakazi
hao zaidi ya 50 wameandamana hadi katika Ofisi za kata na kupokelewa na uongozi
wa kata hiyo akiwemo Diwani Uswege Furika (Chadema) na Ofisa Mtendaji wa kata
hiyo Jumapili Mwasenga huku wakiwa na majembe mikononi wakishinikiza
kuanza kugawiwa eneo hilo.
Awali
ilidaiwa kuwa Diwani huyo aliwaahidi wananchi hao kuwapa eneo kwa ajili ya
biashara ambapo aliwaambia wananchi hao kufika eneo husika asubuhi mapema kwa
ajili ya kila mtu kuoneshwa sehemu yake ambayo angefanyia biashara zake.
Aidha
katika hali isiyokuwa ya kawaida Diwani huyo alipingana na wananchi hali
iliyozua mzozo mkali baina yake na wananchi ambapo alikataa kutoa ahadi
hiyo lakini baada ya kubanwa sana alikubali na kudai kuwa suala hilo
alilifikisha kwa Ofisa Mtendaji wa Kata.
Baada
ya Ofisa mtendaji kupewa nafasi ya kulizungusuala hilo pia alipingana na Diwani
huyo kwa madai kuwa ofisi yake haikuwa na taarifa juu ya ahadi hiyo hivyo
alichokifanya Diwani huyo alipotosha wananchi.
Ofisa
huyo Jumapili Mwasenga alisema suala la Wnanchi kudai eneo la Soko ni madai ya
msingi lakini yana taratibu zake namna ya kuyapata kuongeza kuwa kama Diwani
aliahidi alitakiwa kutoa taarifa Ofisini kwake ili walifanyie utaratibu.
Aliongeza
kuwa pamoja na ahadi hiyo bado yeye kama Mtendaji anatekeleza Ilani ya Chama
cha Mapinduzi na siyo Chama kingine hivyo Diwani alipaswa kupeleka maombi ya wananchi
kwa maandishi ili yafanyiwe kazi.
Kufuatia
majibu hayo yaliyoibua hasira kali kwa wananchi ambao walianza kupiga kelele
wakidai kuoneshwa eneo ili wakaanze kupanga meza tayari kwa biashara
ambapo Mtendaji huyo aliwaahidi wananchi kusubiri ili taratibu zianze
kufanyika ili wapewe eneo hilo.
Wananchi
hao hawakulizika na majibu ya Mtendaji huyo hali iliyopelekea kumbana Diwani
wakidai kuwa hawana imani naye kwa kuwa alikurupuka kutoa ahadi huku akifahamu
utaratibu unaotakiwa kufuatwa kabla ya kuanzishwa kwa soko.
Godfrey
Sanga mkazi wa Mtaa wa Igodima alisema Suala la maendeleo ya kata ya Iganzo
limekuwa likipigwa danadana kila siku ambapo Diwani kupitia mkutano wa chama
cha Chadema uliofanyika Jumapili iliyopita aliwaahidi wananchi hao kuwa wafike kwa
ajili ya kupewa maeneo hali iliwalazimu wananchi kufika eneo hilo wakiwa na
majembe mikononi.
“
Wanatuona kama watoto tusiokuwa na akili huyu diwani yeye mwenyewe aliahidi
kututengenezea barabara na soko alisema lipo eneo tayari sisi tuje ili
kila mtu apewe sehemu yake lakini badala yake anatugeuka” alihoji Hassan
Kasangula mkazi wa mtaa wa Igodima.
Hata
hivyo wananchi hao walionesha kutoridhika na kauli za viongozi hao hali
iliyowalazimu kufika eneo la soko na kuchagua uongozi wa mpito na kuanza
kujigawia tayari kwa kuanza biashara huku uongozi ukibaki unashangaa.
Aidha
kufuatia hali hiyo Diwani huyo alimtupia lawama Mwenyekiti wa Chadema wa kata
hiyo kuwa ndiye aliyetoa ahadi hiyo kwenye mkutano hali iliyosababisha yeye
kulaumiwa na wananchi akihusiashwa na ahadi hiyo.
No comments:
Post a Comment