Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Monday, July 23, 2012

RAIS KIKWETE AZINDUA MRADI WA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA ENEO LA SWAYA MBEYA

RAIS JAKAYA KIKWETE NA KULIA KWAKE NI  KAMISHNA WA UMOJA WA ULAYA KITENGO CHA MAENDELEO ADRIS PIEBALGS  PAMOJA NA BAROZI WA UJERUMANI WAKIKATA UTEPE KWA PAMOJA KUZINDUA MRADI WA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA JIJINI MBEYA



RAIS KIKWETE AKIHUTUBIA WANANCHI WA MBEYA KATIKA UZINDUZI WA MRADI WA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA 

KAMISHNA WA UMOJA WA ULAYA KITENGO CHA MAENDELEO  ANDRIS PIEBALGS AKITOA SALAM ZAKE KWA WAKAZI WA MBEYA KATIKA UZINDUZI WA MRADI WA MAJI SAFI

MKURUGENZI MTENDAJI WA MAJI SAFI NA TAKA  MBEYA MHANDISI SIMEON SHAURI ALIYESHIKA FIMBO AKIMWONYESHA MWESHIMIWA RAIS KIKWETE RAMANI YA MAMBOMBA YA MRADI HUO WA MAJI SAFI JINSI UTAKAVYOWAHUDUMIA WAKAZI WA MBEYA NA VITONGOJI VYAKE

WAZIRI WA MAJI PROF. J. MAGEMBE AKISALIMIANA NA BAROZI WA UJERUMANI  MARA BAADA YA KUWASILI KATIKA MRADI WA MAJI SAFI 

KAMISHNA WA UMOJA WA ULAYA KITENGO CHA MAENDELEO  ANDRIS PIEBALGS AKISALIMIANA NA WAKAZI WA SWAYA MBEYA MARA BAADA YA KUWASILI ENENO LA UZINDUZI WA MRADI WA MAJI SAFI

WABUNGE NA VIONGOZI MBALIMBALI WA CHAMA NA SERIKALI WALIHUDHURIA KATIKA SHEREHE ZA UZIDUZI WA MARADI WA MAJI SAFI

KAMATI NZITO YA MAANDALIZI YA UZINDUZI WA MRADI WA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA MBEYA
WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA

VIONGOZI MBALI MBALI WALIHUDHURIA SHEREHE HIZI


VIKUNDI MBALIMBALI VILIKUWEPO KUTUMBUIZA KATIKA UZINDUZI WA MRADI WA MAJI SAFI

UMATI MKUBWA WA WATU ULIHUDHURIA SHEREHE ZA UZINDUZI WA MRADI HUU WA MAJI SAFI

MC  CHALES MWAKIPESILE AKIONGOZA WIMBO WA TANZANIA NAKUPENDA TANZANIA

MWANDISHI MKUU WA MBEYA YETU JOSEPH MWAISANGO AKIWA KATIKA PILIKAPILIKA ZA KUPATA PICHA NZURI KATIKA UZINDUZI WA MRADI HUO WA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA


Rais Kikweta amezindua mradi mkubwa wa maji uliokamilika kujengwa kwa gharama ya zaidi ya shilingi Bilioni 79.
Akizindua mradi huo, Rais Kikwete aliiagiza Wizara ya Maji kuanza kutafuta vyanzo vipya vya maji kwa ajili ya matumizi ya wakazi wa Jiji la Mbeya na vitongoji vyake vitakavyoanza kutumika ifikapo mwaka 2017.
Alisema kuwa mradi huo kwa sasa unao uwezo wa kuzalisha maji mengi kuliko uwezo wa matumizi ya wakazi wa Jiji la Mbeya na vitongoji vyake.
 Alisema mradi huo unao uwezo wa kuzalisha maji lita za ujazo milioni 51 kwa siku wakati majitaji ya maji kwa wakazi wa Jiji la Mbeya na vitongoji vyake kwa sasa ni meta za ujazo milini 38 pekee.
Hata hivyo alisema kuwa kwa maehesabu ya kitaalam kuhusiana na ongezeko la watu katika Jiji la Mbeya, maji hayo yatakidhi mahitaji hadi mwaka 2017 na kuwa baada ya hapo vyanzo vingine vya mahitaji vitahitajika ili kutosheleza mahitaji ya wakati huo.
“Ifikapo mwaka 2017 tutahitaji vyanzo vingine vya maji, sasa sio vema wakati huo ukifika ndipo tuanze kuvitafuta, naiagiza Wizara ya Maji kuanza sasa kutafuta vyanzo hivyo ili muda huo ukifika tuanze kuvitumia,” alisema Rais Kikwete.
Rais Kikwete alisema kuwa mradi huo umejengwa kwa pamoja kati ya Serikali ya Tanzania iliyotoa Bilioni 29, Umoja wa Ulaya ulitoa Bilini 39 na Ujerumani iliyogharimia shilingi bilioni 13.
Awali akimkaribisha Rais Kikwete, Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe alisema kuwa mradi wa maji  Mbeya kwa sasa ndio mkubwa kuliko yote nchini ambao umejengwa na kukamilika tayari kwa matumizi ya wananchi.
Alisema kuwa Umoja wa Ulaya na Ujerumani pia zimeisaidia Tanzania kujenga miradi ya maji katika mikoa ya Mwanza na , Iringa.
Alisema katika hatua ya pili ya ujenzi wa miradi ya maji nchini sasa itaanza kutekelezwa katika miji ya Bukoba, Mtwara, Lindi, Babati na Musoma.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro alisema kuwa kukamilika kwa mradi huo ni ukombozi kwa wakazi wa Jiji la Mbeya na Vitongoji vyake, ambapo sasa kila mwananchi anao uwezo wa kupata maji safi na salama.
Aliwataka wakazi wa Jiji la Mbeya kulinda na kutunza vyanzo na miundombinu ya maji ili mradi huo uweze kuwa endelevu kwa manufaa ya wananchi wenyewe.

No comments: