Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Tuesday, June 26, 2012

HHOT NUUZ:KIAMA CHA MADAKTARI WALIOGOMA MBEYA KIAMA CHA MADAKTARI WALIOGOMA MBEYA


SERIKALI mkoani Mbeya imetishia kukatisha mikataba ya madaktari watakaoendeleza mgomo mpaka siku ya kesho(Juni 27) ikiwa ni siku tano mfululizo hawajaingia kazini.

Kaimu mkuu wa mkoa wa Mbeya Dk.Norman Sigara ameyasema hayo leo (Juni 26) katika kikao chake na waandishi wa habari ikiwa ni siku ya nne mfululizo tangu baadhi ya madaktari katika hospitali ya Rufaa kuanza mgomo.

Dk.Sigara amesema tangu kuanza kwa mgomo huo serikali ya mkoa kupitia mkuu wa mkoa ambaye kisheria ndiye mwenyekiti wa bodi ya hospitali inayoingia mkataba na madaktari wa mafunzo imeshawaandikia barua za kuwaita ili wafanye mazungumzo lakini jana(Juni 25) hawakufika.

Amesema baada ya kutofika huko mkoa ukawaandikia tena barua kwa kila mmoja wao kujibui ni kwa nini asiwajibishwe na kusisitiza kuwa iwapo mpaka siku ya tano hawatafika kazini mkoa utavunja mkataba na kuwarudisha kwa muajiri yaani wizara husika. 

Amesema kwa sasa wamelazimika kuchukua baadhi ya madaktari kutoka vituo vya afya vilivyopo jijini Mbeya na ndiyo wanaendelea kutoa huduma hususani katika kitengo cha upasuaji cha hospitali ya Rufaa ambacho ndicho kimeathiriwa zaidi.

Kwa upande wake mkurugenzi wa hospitali ya mkoa Dk.Eliuter Samky alisema madaktari waliogoma ni 45 waliopo katika mafunzo na 19 waliosajiriwa lakini wameajiriwa hivi karibuni lakini madaktari bingwa 19 wanaendelea na kazi kama kawaida.

Samky amesema wateja wote waliofika hospitalini hapo tangu kuanza kwa mgomo wameathirika kwa namna moja ama nyingine ikiwa ni kwakupata huduma isiyo katika kiwango ama muda wa kawaida au kisaikolojia.

Amesema tangu kuanza kwa mgomo huo haijatokea kifo lakini wagonjwa 250 wamefikishwa na kulazwa wakati wagonjwa wan je jumamosi walifika 53,jumapili 42 na jumatatu 283.

Amesema siku ya jumapili pia ilitokea ajali ya gari na majeruhi 16 wakafikishwa hospitalini hapo na wote walipata huduma japo si kwa kiwango kilichozoeleka siku zote.

Naye mganga mkuu wa mkoa dokta Seif Mhina alisema mgomo wa madaktari katika hospitali ya rufaa imeongeza msongamano wa wagonjwa katika hospitali ya mkoa hususani akina mama wajawazito waliokwenda kujifungua katika hospitali hiyo kitengo cha wazazi Meta na kukosa huduma ndipo wakaamua kukimbilia hapo.

Mhina amesema wajawazito wanaojifungua katika hospitali ya mkoa wameongezeka kutoka wawili hadi watano kwa siku na kufikia zaidi ya kumi huku wanaopata huduma ya upasuaji wakiongezeka kutoka mmoja kwa siku hadi kati ya watano na kumi.

NAPE AMRUSHIA DONGO LOWASA 
WANACHAMA wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) wametakiwa kutochagua viongozi kwa nafasi zao za kifedha wanazozitumia kurubuni wananchi kwa kutoa misaada mingi.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Nape Nnauye alitoa kauli hiyo leo(Juni 26) alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Mbeya kauli inayoonekana kumhusu moja kwa moja aliyewahi kuwa Waziri mkuu Edward Lowasa ambaye hivi sasa anaonekana kukimbilia makanisani kwa kuchangia harambee mbalimbali.

Baadhi ya wachambuzi wa mambo hususani ya kisiasa wamekuwa wakiitaja njia anayoitumia Lowasa kuwa njia ya kujisafisha na kujitengenezea nafasi nzuri katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Lakini Nape amesema wanaccm wanapaswa wautumie uchaguzi wa chama chao mwaka huu kuhakikisha viongozi wanaomwaga pesa nyingi kwa kutoa misaada wakidhani ni njia nzuri ya kuwashika wapiga kura wanatupwa nje ili kukisafisha chama chao.

Amesema kinachopaswa kufanywa na wanachama ni kuhakikisha wanachagua viongozi walio na uzalendo na chama chao na pia walio na uwezo wa uongozi ili kukijenga chama hicho badala ya kuwapa uongozi watu wanaonyooshewa vidole kila siku na wananchi.

Amewataka vijana hususani walio na elimu kujitosa kupigania uongozi wa chama hicho akisema hatua hiyo itakiwezesha kupata damu change na zilizo na nguvu ya kukiendeleza badala ya kukidumaza.  

Nnauye amekanusha pia kauli za baadhi ya watu wanaokejeli dhana ya Kujivua Gamba wakisema haijafanikiwa kauli aliyosema si kweli kwani dhana hiyo ilibeba mambo mengi ndani yake.

Amesema dhana hiyo ililenga kubadilisura ya chama kwa kuongeza damu change hali inayofanyika hivi sasa ambapo chama kimeanzisha mchakato wa kuwa nam mkoa maalumu kwaajili ya wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu.

Amesema pia kuwawajibisha baadhi ya viongozi wasio na sifa tayari mikakati mbalimbali imefanywa na wapo baadhi ya watu walioachia ngazi mbalimbali pamoja na kuivunja kamati kuu iliyokuwa chini ya Yusuf Makamba.

“Kuna watu wamejivua uanachama mpaka ubunge tumeona leo hii mtu anasema dhana ya Kujivua Gamba haijafanikiwa mi nadhani ni uongo.Lakini pia baada ya chama kutoa muda kwa wahusika wajiwajibishe na hawakufanya hivyo sasa tuna vikao mbalimbali vinavyoendelea kpitia kamati za maamuzi na maadili.Huko nako tutatoka na maamuzi mengine” amesema.

Amesema pia katika uchaguzi mkuu wa chama hicho mwaka huu majina ya wagombea wanaokabiliwa na kashfa mbalimbali hayatarejeshwa hivyo ni vema wanachama hao wasijaze fomu kabisa.
Chanzo: Jodanyp blog

No comments: