Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Wednesday, November 2, 2011

WANANCHI WAMEIFUNGA KWA KUTUMIA MAKUFULI OFISI YA MKURUGENZI WA MAJI - MBLINZI MKOANI MBEYA


Na mwandishi wetu
Wananchi wa Kijiji cha Mbalizi kilichopo wilaya ya Mbeya Vijijini wameifunga kwa kutumia makufuli ofisi ya Mkurugenzi wa Maji safi Mbalizi wakimtaka kuwapatia huduma ya maji ambayo wameichangiwa kwa kipindi cha mwezi mzima.

Tukio hilo limetokea mwishoni mwa wiki baada ya kumalizika kwa mkutano wa hadhara wa kijiji hicho uliokuwa na lengo la kusoma mapato na matumizi ya kijiji.

Wakati afisa mtendaji wa Kijiji hicho Malongo Sumuni akisoma taarifa ya mapato na matumizi wananchi wa kijiji hicho walimtaka afisa mtendaji kutoendelea na ajenda ya ugawaji wa vocha za Ruzuku na badala yake walimtaka kuwaeleza hatma yao ya kupata huduma ya maji safi.

Kutokana na kauli hizo zilizokuwa zikitolewa na wananchi mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Mbeya Vijijini William Simwali aliwataka viongozi wa idara ya maji kuwa wakweli kwa wananchi badala ya kuumba maneno ili waweze kujipatia kipato isivyo halali.

Hadi tunaingia mitamboni leo hii ofisi ya mkurugenzi wa idara ya maji wilaya ya Mbeya Vijiji bado ilikuwa imefungwa kwa kufuri.

No comments: