Na mwandishi wetu.
Bwana Tedi Broun mwenye umri wa miaka 22 mkazi wa Katumba wilayani Rungwe mkoani Mbeya amefariki dunia baada ya kupigwa na wananchi wenye hasira kali wakimtuhumu kuiba mbao.
Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Anecletusi Malindisa amesema mtu huyo amefariki dunia jana majira ya saa moja za asubuhi wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya wilaya ya Rungwe.
Amesema marehemu alikuwa akituhumiwa kuiba mbao mbili zenye thamani ya shilingi elfu 8 mali ya Aliko Mwasandube, hata hivyo hakuna mtu aliyekamatwa kuhusika na mauaji ya mtu huyo.
Aidha kaimu kamanda Malindisa ameitaka jamii kuachatabia ya kujichukulia sheri mkononi na badala yake amewataka kumfikisha mtuhumiwa katika kituo cha polisi ili aweze kuchukuliwa hatua zaidi za kisheria.
No comments:
Post a Comment