Na mwandishi wetu
Wakazi wa halmashauri ya Lupa wilaya ya Chunya mkoani Mbeya walazimika kutembea umbali mrefu wa kilometa 5 kufuata maji safi na salama kufuatia ukame unaoikabili halmashauri hiyo kutokana na sababu za mabadiliko ya tabia ya nchi.
Wakiongea na mwandishi wetu wananchi hao wamesema kuwa licha ya kuwepo kwa visima vilivyochimbwa na serikali wameendelea kukabiliwa na tatizo hilo, kwani visima hivyo vimekauka kwa sababu ya kuchimbwa katika maeneo yasiyo na maji.
Mmoja wa wakazi hao Bi Recho Paskal amesema maji yanayopatikana hivi sasa wanayachota kwenye mto Lupa na kwenye visima vinavyochimbwa kiasili.
Naye mkurugenzi wa taasisi inayohusika na utunzaji wa misitu asili ya Kaeya Bwana Lukas Malangalila amesema ufugaji holela na kilimo kizichozingatia kanuni za kilimo maeneo yenye vyanzo vya maji umechangia kwa kiasi kikubwa tatizo la maji licha ya kuwepo kwa mabomba ya kupitishia maji safi yaliyowekwa na serikali.
No comments:
Post a Comment