Afisa mtendaji wa mtaa wa Maendeleo kata ya Iyunga jijini Mbeya Bi Tabu Sengo Tabu ambaye ametapeliwa simu yekye thamani ya shilingi 90,000/= kijana mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Geogre Ramsi aliyedai kuwa ametokea jijini Tanga, alifika katika uongozi wa serikali hiyo kuomba msaada wakumzika ndugu yake aliyedaiwa amejifungua na kufariki katika Hospitali ya Rufaa Meta jijini hapa.
Bwana Elias Mwakyusa aliyeitwa kusaidia kuzika akiwa amefika kwa fundi seremala kubeba misalaba.
Dereva akiwa na pikipiki iliyokodiwa na kijana tapeli George Ramsi aliyedai kufiwa na ndugu yake aliyejifungua katika hospitali ya Rufaa Meta kwa njia ya operasheni ambaye naye alitapeliwa simu yenye thamani ya shilingi 80,000/= za kitanzania na fedha zilizokuwa katika akaunti ya MPESA shilingi70,000/=
Vijana wa kutoka kushoto ni Obadia Robert Kyando, Obby Mwakasasagule, Shida Mwasambili na Matatizo Kyando waliokodiwa kwa ajili ya kuchimba kaburi kwa shilingi 110,000/= ambapo waliahidiwa kulibwa na kijana huyo baada ya mazishi lakini hawakuweza kulipwa.
Fundi seremala Maiko Mwakalonge aliyefika katika ofisi ya Afisa mtendaji Bi Tabu Sengo kutoa malalamiko ya kutengeneza misalaba na mteja wake kutoonekana.
Kijana huyo tapeli George Ramsi ametokomea kusikojulikana baada ya kupelekwa kwa Mchungaji wa kanisa la Sabato Nzovwe, majira ya saa saba akiomba taratibu za mazishi kufanyika katika kanisa lake, kitu ambacho si cha kweli na kudai anaomba kwenda kununua vocha ndipo alitokomea moja kwa moja na simu ya afisa mtendaji, dereva wa pikipiki na shilingi elfu mbili ya dereva taksi.
1 comment:
Ilikuwaje hao jamaa wakatoa cmu kwa mtu wasiyemjua....!!? Kama vipi Kuna uzembe ndani yake, sasa kazi kwao kusaidiana na polisi kumsaka jamaa..!! NA kusisitiza polisi jamii kwenye maeneo Yao...!! Nawapa pole sana kwani jamaa kawarudisha nyuma...!!
Post a Comment