Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Sunday, October 30, 2011

GHARAMA ZA MAJI WILAYANI RUNGWE MKOANI MBEYA KUPUNGUZWA

Mkuu wa wilaya ya Rungwe Mh. Jackson Msome.
*****
Na Gordon Kalulunga.
Serikali wilayani Rungwe Mkoani Mbeya imesema tatizo la kupanda ghafla kwa bei za maji wilayani humo limefanyiwa kazi na kwamba Mamlaya ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura) imeanza kushughulikia na kushusha gharama hizo.

Hayo yalielezwa na Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Jackson Msome
wakati akizungumza na wazee wa wilaya ya Rungwe, Wachungaji na wajumbe wa Kamati ya Ulizi na Usalama ya wilaya hiyo katika mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa Community Center mjini Tukuyu.

Msome alisema
baada ya kuwepo kwa malalamiko mengi ya wananchi aliamua kulishughulikia tatizo hilo kwa ushirikiano na wajumbe wanne kutoka wilayani humo kwenda Jijini Dar es Salaam kuonana na Meneja Mkuu wa Ewura, Haruna Masebu kwa ajili ya kumfikishia kilio cha Wananchi.

Alisema mazungumzo baina ya ujumbe wake na Meneja wa Ewura yalikuwa magumu, lakini hatimaye kwa pamoja walifikia njia muafaka ya kufanya ili kupunguza gharama za maji ambazo zimeonekana kugomewa na wananchi kutokana na kuwa na ongezeko kubwa la zaidi ya aslimia 125 kwa mara moja.


Alisema njia waliyoafikiana na Masebu ni kwa Meneja wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Rungwe kupangua bajeti yake pamoja na baadhi ya mikakati yake ili kutoa mwanya wa kushusha Ankara za maji kwa wakazi wa Rungwe.


Mkuu huyo wa Wilaya alisema hadi sasa Meneja wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Rungwe, yupo Jijini Dar es Salaam akisaidiana na wataalam wa Ewura kushughulikia suala hilo.


“Kikundi kidogo cha waanasiasa wamejitumbukiza katika suala hili na kudai kuwa wao ni wakazi wa kata saba za Tukuyu na wamekuwa wakitumia vyombo vya habari kusema kuwa mara wataniburuza mahakamani, wakati mwingine wakimtaka Rais anihamishe na sasa wanataka asinihamishe bali aninyang’anye ukuu wa wilaya, hawa ni wachochezi” alisema
Msome.

Alisema tuhuma wanazomwelekezea kuwa ameamuru Polisi kuwakamata viongozi wanaohamasisha wananchi kutolipia Ankara za maji si za kweli, kwani yeye aliyochokifanya ni kupiga marufuku mikutano isiyofuata taratibu na sheria za nchi pamoja na michango wanayowachangisha wananchi bila kuwa na kibali cha Serikali.

''Walipokaidi amri halali ya Serikali ndipo walipokutana na mkono wa dola, sasa wanadai kuwa ni mimi niliyewatuma Polisi kuwakamata ili kuzuia mikutano yao” aliongeza Mkuu wa wilaya huyo.

Alisema ikiwa watu hao wanahitaji kufanya mikusanyiko halali wafuate taratibu kwa kuomba kibali cha Polisi na hata kama wanataka kuchangisha wananchi waombe kibali ili fedha hizo ziweze baadaye kukaguliwa ikiwa zitatumika kinyume na malengo waliyoainisha.

“Tukiwaacha wawachangishe wananchi kiholela kama wanavyotaka wao itaibuka DECI nyingine hapa na Serikali ndiyo itakayolaumiwa na wananchi” alisema.

Katibu wa wazee wa Wilaya ya Rungwe Ambakisye Mwakatobe alisema kuwa wazee wa Rungwe bado wanamuhitaji Musome kutokana na utendaji wake wa kazi na kuwa kikundi kidogo cha watu saba hakiwezi kuwakilisha mawazo ya wana Rungwe wote.

No comments: