Baadhi ya Warembo wa Vodacom Miss Higher learning waliokuwa katika ziara ya kutembelea Makao makuu ya Vodacom Tanzania yaliyopo Mlimani City jijini Dar es salaam ambapo shindano lao linatarajiwa kufanyika mwishoni mwa wiki mjini Dodoma.
Mmoja wa warembo wa Vodacom Miss Higherlearning akimuualiza Meneja wa Vodashop Mlimani City Bi. Fatma Kalyanye swali juu ya huduma zinazoedeshwa na vodashop pindi walipozuru Makao makuu ya Kampuni hiyo jana.
Meneja wa Vodashop Mlimani city Fatma Kalyanye akiwaelekeza warembo wa Vodacom Miss higher learning waliozuru duka hilo namna ya kuweka nyaraka za kudumu za wateja wao wa M pesa,warembo hao walitembelea makao makuu ya kampuni hiyo ikiwa ni moja ya hatua za kuelekea kilele cha shindano lao liatakalofanyika mwishoni mwa wiki mjini dodoma.
Mfanyakazi wa Vodacom Tanzania kitengo cha huduma kwa wateja Bw. Hiramu Mungai akitoa ufafanuzi wa jinsi ya kutoa huduma kwa wateja kwa Warembo wa Vodacom Miss higherlearning waliokuwa katika ziara ya kutembelea makao makuu ya kampuni hiyo jana.
Mfanyakazi wa Vodashop Mlimani City Jane Mrosso Akiwapa maelekezo ya matumizi ya simu mbalimbali baadhi ya warembo wa Vodacom Miss Higher learning walipotembelea duka hilo hapo jana,ikiwa ni hatua mojawapo ya kuelekea katika shindano lao linalotarajiwa kufanyika mwishoni mwa wiki mjini Dodoma.
Mkuu wa kitengo cha huduma kwa wateja wa Vodacom Tanzania Najenjwa Mbaga akisalimiana na warembo wa Vodacom miss higherlearning walipozuru makao makuu ya kampuni hiyo jana wakiwa safarini kuelekea mjini Dodoma katika fainali za shindano lao litakalofanyika mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya Warembo wa Vodacom Miss Higher learning wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza ziara yao ya kutembelea Makao makuu ya Vodacom Tanzania yaliyopo Mlimani City jijini Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment