Mrembo aliyeshinda taji la Miss Universe Tanzania 2011 Nelly Kamwelu ameshinda taji la Miss Southern Afrika International 2011 katika mashindano yaliyofanyika Ndola nchini Zambia na kushirikisha warembo kutoka nchi mbalimbali za kusini na mashariki mwa Afrika.
Nelly aliyepata mwaliko wa kushiriki mashindano hayo kupitia bodi ya Utalii Tanzania (TTB) ameshinda taji hilo jumapili ya Juni 27 mwaka huu.
Fursa hiyo imemsaidia Nelly kupata uzoefu kabla ya kwenda katika mashindano ya Miss Universe kimataifa mwezi wa nane na tisa mwaka huu.
Mashindano hayo mbali ya kujenga mshikamano miongoni mwa nchi za kiafrika yanalenga pia kuvutia na kutangaza utalii wa nchi washiriki.
Mbali na kuhsiriki shindano la urembo,wakiwa nchini Zambia warembo washiriki akiwemo Nelly walihsiriki na kufanya kazi mbalimbali za kijamii kama vile kutembelea hospitali za watoto na vituo vya kulelea watoto na kushiri maonyesho ya kimataifa ya biashara nchini humo.
Ukiondoa Tanzania nchi nyingine za Afrika zilizoshiriki ni Namibia, Zambia, Lesotho, Afrika ya Kusini, Botswana, Zimbabwe, Swaziland, Congo, Malawi na Msumbiji.
Nyota ya Nelly ilianza kung’ara pale aliposhinda taji la Miss Universe katika shindano lililodhaminiwa na kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania ikiwa ni sehemu ya azma ya kampuni hiyo ya kuibua,kuendeleza na kulinda vipaji vya vijana wa kitanzania katika sanaa na michezo.
Azma hiyo inalenga kuwapatia fursa vijana ya kujiendeleza kimaisha kupitia vipaji pamoja na kutimiza ndoto walizonazo katika sanaa.
Kwa kushikilia taji la Miss Southern Afrika Internation Nelly anawajibu wa kutoa elimu kwa jamii juu ya saratani ya matiti na mfuko wa uzazi na atakuwa balozi wa nia njema wa mtandao wa saratani ya matiti na mfuko wa uzazi Zambia.
Aidha ushindi huo umempatia Nelly pamoja na zawadi mbalimbali mshahara wa kwacha millioni moja kwa mwezi kwa kipindi cha miezi kumi na minne.
No comments:
Post a Comment