Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Friday, July 29, 2011

MATUKIO YALIYOJIRI BUNGENI DODOMA KATIKA PICHA LEO

Naibu Spika Job Ndugai (wa pili kutoka mbele) akiingia bungeni leo kwaajili ya kuanza kikao cha thelathini na sita katika mkutano wa nne wa bunge unaoendelea mjini Dodoma.Picha na Anna Nkinda - Maelezo
Waziri wa Ujenzi Dk. John Magufuli (katikati) akifurahia jambo na Mbunge wa Vunjo (TLP) Augustino Mrema(kushoto) na Mchungaji Israel Natse (CHADEMA) (kulia) Mbunge wa Karatu kabla ya kuanza kwa kikao cha thelathini na sita katika mkutano wa nne wa bunge unaoendelea mjini Dodoma.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda (kulia) akiongea jambo na Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-MAGEUZI) David Kafulila (kushoto) leo katika kipindi cha maswali na majibu kwenye Mkutano wa nne wa Bunge unaoendelea mjini Dodoma.
Mbunge wa Bumbuli (CCM) January Makamba akimuuliza swali waziri wa Nishati na Madini kuwa Serikali inamapango gani wa kuendeleza mradi wa umeme katika kata ya Mgwashi leo katika kipindi cha maswali na majibu kwenye Mkutano wa nne wa Bunge unaoendelea mjini Dodoma.

Mbunge wa Mtera (CCM) Livingstone Lusinde akitoa mwongozo kwa Mwenyekiti wa Bunge wa kikao cha thelathini na tano kilichofanyika jana mjini Dodoma Jenista Mhagama (hayupo pichani) kuwa wabunge wate wakapimwe akili hii ni kutokana na matukio ya uvunjifu wa kanuni yanayotokea mara kwa mara ndani ya Bunge.

No comments: