Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Sunday, July 31, 2011

Kikundi cha mchiriku cha jagwa music toka tandale chawasha moto denmark

Mpiga kinanda wa muziki wa Mchiriku wa Jagwa Music group toka Tandale jijini Dar es salaam kikitumbuiza usiku wa kuamkia leo katika jijini Copenhagen, nchini Denmark, ambako wamepagawisha wapenzi wa muziki wa mchiriku isivyo kawaida. Karibu kila mwaka kundi hili hualikwa katika matamasha mbalimbnali ughaibuni. Wao hawana makuu, vvyombo vyao ni hicho kinanda, ngoma, filimbi na kiti cha kukalia ambacho hufanywa percussions. Wakianza hakuna anayebaki ameketi na wana uwezo wa kupiga muziki usiku kucha bila kuchoka
Add captionMwimbaji wa Jagwa akighani na kumfanya mshabiki ashindwe kujizuia
Mnenguaji wa Jagwa Music band ilibidi ashikiwe kiti
Mcheza show wa Jagwa akifanya vitu vyake.
PICHA KWA HISANI YA VIJIMAMBO BLOG

No comments: